CELG LAIBUA UKATILI KITETO


CELG laibua ukatili Kiteto
 
Na Mohamed Hamad Manyara
Kituo cha utawala wa sheria za mazingira CELG chini ya ufadhili wa legal services facility kimeibua aina za ukatili unaowakabili wananchi wilayani Kiteto mkoani manyara unaotokana na mfume dume

Wakiwa katika mafunzo na kikundi cha akinamama mjini kibaya walisema miongoni mwa ukatili uliokithiri Kiteto ni pamoja ukatili wa kingono,kiuchumi,

Akiwasilisha mada ya ukatili wa kijinsia afisa utawala fedha wa shirika la CELG Emmanuel Mgalla alisema utafiti uliofanywa hivi karibuni umebaini wilaya ya Kiteto,Babati,Mbulu na Hanang mkoani Manyara ni vinara wa ukatili wa aina mbalimbali

"Tmeshuhudia wanawake wakifanyiwa ukatili wa vipigo,ngono,na hata ule wa kipigo jambo ambao sasa limepitwa na wakati akisema tabia hizo zife mara moja

Alisema kutokana na hali hiyo shirika limeamua kutoa elimu katika Maeneo tofauti yakiwemo shule za sekondari vikundi ndani ya jamii wakiwemo wajane na wasaidizi wa kisheria ili kuvipunguza

"Huu utakuwa ni mradi wa miaka miwili ambao tutahamasisha kupunguza ukatili wa kijinsia uliokithiri katika maeneo hayo ambayo wanajamii za wakulima na wafugaji"

Akichangia mada hiyo Amina Malekela (mjane) alisema ukatili Kiteto ni mkubwa kutokana na mila na tamaduni za wakazi wa maeneo hayo

Alisema hali hiyo inachukuliwa kama mazoea ya wanaume kupiga wake zao kudhulumu haki za wenzi wao kutokana na mfumo dume uliopo

"Tumeamua kumwachia mungu baada ya serikali kushindwa kudhibiti vitedo hivi kupitia idara zake" alisema
Kwa upande wake Hawa Swalehe mshiriki akitoa ushuhuda huku akiangua kilio alisema baada ya mume wake kufariki alinyanyaswa na ndugu wa mume hadia akakata tamaa

Alisema katika ukatili huo kwa wenye waume zao mbali na vipigo, Watoto kutelekewa wamekuwa wakiteremshwa hâta kwenye vitanda kwa madai kuwa hawajaja navyo

Katika kukabiliana na ukatili huo shirika hilo limewataka akinamama hao kuungana pamoja ili waweze kujengewa uwezo wa kudai haki zao pamoja na kusomesha watoto

Mwisho








Maoni