CELG:Manyara yaongoza kwa ukatili 71%
·
Wanafunzi Sekondari Babati walaani ukatili
huo
NA.MOHAMED HAMAD MANYARA.
Tafiti zilizofanywa na mashirika yasiyokuwa ya
kiserikali hapa nchini ikiwemo Wizara ya Afya mwaka 2013 imebainika kuwa mkoa
wa Manyara unaongoza kwa vitendo vya ukatili kwa 71% dhini ya mikoa mingine
Wizaya ya Afya ilifanya utafiti mwaka 2013 kuwa mkoa wa
Manyara unaongoza kwa ukatili wa ukeketaji kwa 71%,Dodoma kwa 64%, Arusha
59%,Mara 40,Morogoro 21, na Tanga 20% ambapo CELG imeamua kuingilia kati ili
kuutokomeza
Kituo cha utawala wa sheria na mazingira (CELG) chini ya
ufadhili wa LSF kutokana na tafiti hizo kimeweka kambi katika wilaya za
Kiteto,Babati,Mbulu na Hanang mkoani Manyara ili kukabiliana na ukatili huo
ambao umedaiwa kuwa tishio kwa jamii hizo
Awali akielezea malengo ya kituo hicho jana mbele ya
wanafunzi kutoka shule za Sekondari Kwaraa,Babati day na Eloni Sekondari mwezeshaji toka kituo cha CELG
Emmanuel Mgalla alisema madhara ya ukatili yamezidi kujitokeza kutokana na
sababu mbalimbali zikiwemo za wananchi kukata tama na kuendekeza ukatili huo
Alitaja aina za ukatili huo kuwa ni ukatili wa Kiuchumi, kisaikolojia, kimwili na kiroho
ambao amedai umekuwa tishio hapa nchini na kuleta madhara ya jamii kwa wananchi
kukata tamaa ya maisha baada ya kukosa mahitaji yao muhimu kwa wakati
Akichangia mada hiyo Edith Nelson mwanafunzi wa Babati Day
Sekondari alitaja madhara yatokanayo na ukatili huo kuwa ni pamoja na
kuathirika kisaikolojia,vifo kutokana na ukeketaji,ulemavu wa kudumu,ongezeko
la watoto wanaoishi mitaani,magonjwa ya zinaa yanayotokana na ubakaji na Ukimwi
Alisema hali hiyo imechangia jamii kuingia katika mfumo
mbovu wa maisha ambao unaleta madhara makubwa na kuilazimu Serikali kufanya
kazi ya ziada kukabiliana na vitendo vya kihalifu ambavyo ilikuwa kwao rahisi
kukabiliana navyo kwa njia ya kuealimisha umma kuepukana navyo
“Tunashuhudia Serikali ikipambana na wahalifu wa aina
mbalimbali wakiwemo vibaka,wauaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi
Albino,majambazi,na kila aina ya uhalifu haya ni matoko ya ukatili uliokwisha
fanyiwa watu hao na sasa wanalipiza visasi”alisema
Aina nyingene ni kushuka kwa kiwango cha elimu kwa wanafunzi
mara wazazi wanapoachana, mmomonyoko wa maadili ndani ya familia, mimba
zisizotarajiwa kusambaratika kwa familia na wazazi kulipa visasi kwa watoto wao
kuwapa mateso mara wanapowazaa
Kwa upande wake Nenduvoto Wilson (mwanafunzi) wa Babati
day Sekondari alitaja madhara mengine kuwa ni pamoja na kupungua kwa nguvu kazi
ya Taifa kwa wahanga kupata vilema vya kudumu kama vile kukatwa viungo vya
mwili hivyo kuwa tegemezi kwa jamii
Naye Nice Zacharia mwanafunzi wa Babati day aliitaka
jamii kuacha kuwa na mtazamo hasi wa kuelimisha watoto kwa ubaguzi hasa wa kike
kukosa fursa hizo adhimu kwa madai ni wakuolewa tu na sio kufanya kazi kama
walivyo wa kiume
“Ubaguzi huu uko katika nyanja mbalimbali zikiwemo shuleni
mtoto wa kike akitaka uongozi inatafsiriwa kuwa anataka kufanya kazi ya kiume ili
hali kuna ushahidi unaoonyesha mafanikiwa makubwa katika kazi mbalimbali
wafanyazo wanawake nchini”alisema
Maoni
Chapisha Maoni