Kiteto
yamnyima usingizi Pinda
Na.Mohamed Hamad Manyara
Mauaji yanayoendelea kujitokeza kila mara kati ya
wakulima na wafugaji wilayani Kiteto mkoani Manyara yamedaiwa kumnyika usingizi
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano Mizengo Kayanza Pinda
Hayo yameelezwa na Kanal Kininyang’ombe Nzoka Mkuu wa
Wilaya ya Kiteto aliyeshika nafasi ya Martha Jaki Umbulla wakati akiwasilisha
taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM 2014/2015 kuwa imetekelezwa kwa zaidi ya
75%
“Wilaya ya Kiteto
imekuwa na majina mengi, imeitwa Somalia na majina mengine ya maeneo yenye vita
kutokana na mauaji yanayoendelea kujitokeza naomba uwepo wangu uchukuliwa
kutaka kukomesha migogoro hii”
“Nitafanikiwa endapo nitapata ushirikiano wa kutosha
kutoka kwenu ambao utaleta mahusiano mema kati ya wakulima na wafugaji kama jitihada
zinavyoendelea kufanywa na mamlaka mbalimbali zikiwemo tume zilizoundwa na
uongozi wa juu”alisema
Hata hivyo migogoro hiyo imetajwa kuwa na changamoto
nyingi zikiwemo zile za ukabila,rushwana hata kutowajibika kwa baadhi ya
viongozi katika nafasi zao huku wananchi wakiendelea kupoteza maisha
Katika kikao hicho cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa
Ilani ya CCM baadhi ya wajumbe walihoji kutokamilika kwa baadhi ya miradi huku
kukiwa na changamoto za ukosefu wa fedha
Serikalini toka kwa baadhi ya viongozi
Akijibu hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Halamshauri ya
Wilaya Bosco Ndunguru aliwatoa wasiwasi wajumbe hao kuwa bado kuna muda wa
kutosha kukamilisha miradi hiyo hadi mwezi wa wasaba ambao ndio unakamilika
mwaka wa Serikali
Hata hivyo baadhi ya wananchi waliozungumzia miradi hiyo
walisema bado kuna changamoto nyingi katika upatikanaji wa huduma za jamii
zikiwemo maji afya na elimu kuwa Serikali ijipange katika kuondoa mapungufu
hayo
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni