mwandishi wa habari Mohamed Hamad akifanya mahojiano na mwathirika wa masuala ya ukatili huko Babati Manyara
Mwanamke
akatwa kiganja na hawara Babati
Na. Mhomaed Hamad Manyara
Utatili wa kijinsia unazidi kuchukua sura mpya mkoani
Manyara ambapo mwanamke Fausta Marandu (35) mkazi wa kijiji cha Duru wilayani Babati
vijijini amekatwa kiganja chake hadi kudondoka na mtu aliyedaiwa kuwa ni hawara
yake
Mwanamke huyo alijitokeza mbele ya watoa maamuzi wakiwemo dawati la jinsia la Polisi,watumishi wa mahakama,viongozi wa Serikali, mashirika ya Dini pamoja na mashirika ya umma kwaajili ya kutafuta ufumbuzi wa
masuala ya ukatili yanayoendelea mkoani humo
Mafunzo hayo ya siku moja yaliyolewa na CELG chini ya
ufadhili wa LSF ambapo pamoja na mambo mengine yalilenga kukumbushana wajibu wa
kila mmoja katika kukabiliana na ukatili wa kijinsia
Wakati mafunzo hayo yakiendelea alijitokeza mwanamke
Fausta akiwa ameshikilia kiganja chake na kuomba msaada wa kupata ulinzi dhidi ya hawara yake huyo ambaye kwa sasa anamwinda kutaka kumuua baada ya kutimiza adhma ya kumtia kilema kwa kumkata kiganya
Tukio hili lilitokea feb 12 mwaka 2011 ambapo hawara huyo alimkata kiganya chake hicho hadi kudondoka kisha kuahidi kutaka kumuua kutokana na ulevi uliopindukia kisha kukamatwa na kufikisha mahakamani ambapo hapo alifungwa jela miaka saba na
baadaye kuachiwa huru baada ya miaka mitatu
“Kwa sasa naishi maisha ya taabu na shida kubwa kwani Migire
Amri mtu niliyekuwa naishi naye kama hawara ameapa kutaka kuniua kila siku
ananiwinda nimetoa taarifa Polisi hakuna msaada nilioupata naombeni msaada ndugu zangu”alisema mama huyo
Akiongea huku akionyesha kiganja chake
ambacho kimedaiwa kukaushwa kwa moto kama kielelezo alidai malalamiko yake
yamefikishwa kituo kidogo cha Magugu bila mafanikio
Hata hivyo watoa maamuzi hao kwa pamoja waliweza kumsaidia
kiasi kidogo cha fedha kisha kuambatana naye hadi kwa mkuu wa kituo cha Polisi Babati
ambapo hapo walihakikishiwa Jeshi la polisi linafuatilia kujua hatma yake
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni