Mwenyekiti CHADEMA Monduli akanusha kuahamia CCM
Na MOHAMMED SHAABAN MONDULI
MWENYEKITI wa chama cha
Demokrasia na maendeleo CHADEMA wilayani Monduli Japhet Sironga amekanusha
uvumi wa kisiasa kuwa amehamia CCM wakati wa ziara ya katibu mkuu wa CCM Abrahaman
Kinana akiwa mkoani Arusha
Hatua hiyo imefikiwa na
mwenyekiti huyo baada ya wanachama wake kuendelea kumhoji juu ya uvumi huo
ambao alidai kuwa sio kweli na anashangaa kusikia kuwa amehama chama tena kupitia mikutano ya CCM
“Ninachofahamu kuna bwana
mmoja aliyewahi kuwa mwenyekiti wa CHADEMA Mch.Amani Silanga maarufu Ole Njakai
ndiye aliyetangaza kujiunga na CCM baada ya kufukuzwa na CHADEMA na kuvuliwa
nyazifa zake zote”alisema Sironga mwenyekiti wa CHADEMA Monduli
“Huyu bwana ifahamike kuwa
alifukuzwa uanachama toka Nov 17 mwaka 2013 na kuvuliwa nyazifa zote ndani ya chama
baada ya kuonekana kufanya hila za kutaka kukihujumu chama”alisisitiza Sironga
Baadhi ya nyazifa alizokuwa nazo
ni pamoja na uenyekiti wa chama Wilaya na mjumbe wa mkutano mkuu wa CHADEMA
Taifa ambazo alizipata kwa kuaminiwa na wanachama kushikilia
Bw. Sironga aliwataka
wanachama hao kuepuka majungu na propaganda za kisiasa ambazo zinatapakazwa na
wanaCCM kuwa Monduli hakuna CHADEMA wala wanachama akisisitiza kuwa chama
kimeenea kata zote 20 za wilayani Monduli
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni