RC Manyara azindua mradi wa maji wa 134.1 mil
NA.MOHAMED HAMAD KITETO
MKUU wa Mkoa wa Manyara Dr
Joel Bendera amezindua mradi wa maji wa kitongoji cha Kona kijiji cha Kijungu wilayani
Kiteto mkoani Manyara ambao utanufaisha wakazi 3,078 wa kata ya Kijungu ambao
walitaabika na huduma hiyo
Mradi huyo wenye thamani ya
134,107,000 umejengwa chini ya mpango wa maji vijijini WSDP kwa ushirikiana wa
Serikali ya Tanzania
na Benki ya Dunia kwa lengo la kukabiliana na uhaba wa maji vijijini
Ikisemwa risala kwa mgeni
rasmi ilieleza mradi huo umehusisha ujenzi wa nyumba moja ya
mashine,mbauti,tanki la ujazo wa mita 50,ujenzi wa nyumba moja ya mlinzi,vituo
3 vya kuchotea maji,ununuzi na ufungaji wa genereta moja ya umeme na pampu na
kutandaza mabomba
Kwa mujibu wa Jemsi
Kionaumela Mhandisi wa maji wilaya alisema mradi huo umekamilika na utawanufaisha wananchi wa
vijiji zaidi ya vitatu na vitongoji vyake wapatao 3078 katika kata ya Kijungu
“Mheshimiwa mkuu wa mkoa
mradi huu umekamilika una uwezo mkubwa wa kuwaondolea adha wananchi wa maeneo
haya ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakitaabika na tatizo la maji na kushindwa
kufanya shuhuli zingine za maendeleo”alisema Eng.Jemshi Kionaumela
Kwa upande wa wananchi wa
kitongoji hicho cha kona walimweleza mkuu huyo wa mkoa kuwa ndoa zao ziliyumba
kutokana na kutoaminiana kwa wanadoa kutokana na wanawake kutumia muda mwingi
kusaka maji
“Tulikuwa tukipigwa na waume
zetu wakati mwingine tunapochelewa kurudi nyumbani na hii sio kutokana na
michepuko bali ni kwa kuchelewa kupata maji sambamba na wivu wa mapenzi kwa
waume zetu” alisema mmoja wa wanawake kijijini hapo
Akihutubia wananchi hao Dr
Joel Bendera aliwataka wananchi hao kulinda mradi huo wa maji ambao ni adhimu
akisema kuna hulka za watu ambao hata Mungu anawajua kuwa wanatabia ya
uchokonozi kama akina tomaso
“Hapa kuna akina thomaso
hawakosekani,nemeambiwa mradi huu ulianza kuhujumiwa sasa naagiza mtu yoyote
atakaye hujumu mradi sheria kali zitachukuliwa dhidi yake kwani hatuwezi
kuwavumilia watu wa aina hii”alisema
Awali katika kile
kilichodaiwa kushangaza viongozi na wananchi wengi mtu ambaye hajafahamika siku
chache kabla ya uzinduzi aliweka chumvi kwenye mashine hiyo ya maji ili
isifanye kazi jambo ambalo liliibua hisia tofauti kwa wakazi
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni