RC Manyara kuzindua mradi wa maji uliohujumiwa


RC Manyara kuzindua mradi wa maji uliohujumiwa
·       
                          Mashine yatiwa chumvi,mlinzi mbaroni
Na Mohamed Hamad Manyara
MKUU wa mkoa wa Manyara Dr Joel Bendera anakusudiwa kufungua mradi mkubwa wa maji kitongoji cha Kona Wilayani Kiteto uliohujumiwa kwa mashine yake kutiwa chumvi ili usifanye kazi kutokana na mgogoro wa wananchi uliodumu kwa muda mrefu bila ufumbuzi

Mradi huo ulijengwa chini ya ufadhili wa benki ya dunia na Serikali ya Tanzania ambapo gharama zake kuanzia mwanzo wa mradi zilikadiriwa kuwa zaidi ya 300 milion zikilengwa kusaidia vijiji zaidi ya vitatu vinavyozunguka mradi

Mkuu wa mkoa wa Manyara Dr Joel Bendera anakusuiwa awe mgeni rasmi tar 22 feb mwaka huu kwaajili ya kuuzindia baada ya kukamilika ambapo kwa mujibu wa taarifa toka uongozi wa Wilaya mradi umegharimu mil 137 hadi kukamilika

Kutokana na mgogoro toka mradi huo uanze mara baada ya kkamilika mradi huo ukahujumiwa kwa kuwekwa chumvi na mtu ambaye hajajulikana kwenye tanki la mafuta na kwenye filta ili usiweze kufanya kazi

“Walipotaka kuwasha mashine wahudumu asubuhi haikuwezekana tukaitwa na baada ya kufungua baadhi ya maeneo kwenye filta tulikuta kuna chumvi na kwenye tanki la mafuta nako”alisema Eliasi Challo mweka hazina wa mradi  huo wa maji kona

Alisema baada ya hapo walitoa taarifa wilayani ambako hapo walipata maagizo yakiwemo kukamatwa kwa mlizi aliyejulikana kwa jina moja la Johanis kwaajili ya mahojiano zaidi ambapo hadi leo siku ya tatu bado anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi alisema Challo

Baadhi ya vijiji vilivyolengwa kunufaika na mradi huo ni pamoja na Kijungu,Ngapapa,Amei,Lerug,na Kisima ambavyo vimezunguka eneo la maradi huo ambao kwa sasa umehujumiwa na haijulikani mfumo utakaotumika kuuendesha kutokana na hujuma hizo

Uongozi wa wilaya ukizungumzia sakata hilo walisema jitihada za kuurudisha mradi katika hali yake zinafanyika na utazindulwa tar 22 na mkuu wa mkoa wa manayara ambapo lengo nikuhakikisha wananchi wananufaika na mradi huo

Utafiti uliofanywa na gazeti hili umebaini chanzo cha hujuma hizo kuwa ni kujengwa mradi huo eneo ambalo wanufaika hawatakiwi kupita kwenye shamba la mmoja wa wananchi hao ambaye amelima na kupanda mazao yake

Toka mwanzo tulisumbuana sana na Yule bwana hataki watu wapiti shambani kwake na hata wakati mwingine tuliweza kushirikisha viongozi akiwemo diwani na wengine wengi lakini ilishndikana”kilisema chanzo kimoja cha habaro hizi

Mwisho

Maoni