Picha na Mohamed Hamad Manyara
Viongozi
vihiyo chanzo cha matatizo Nchini.
Na Mohamed Hamad Manyara.
Usaliti wa baadhi ya viongozi wa Serikali na vyama vya
Siasa hapa nchini wa kutotenda majukumu yao ipasavyo ndani ya jamii umetajwa
kuwa ni moja ya matatizo yanayolilikumba Taifa katika kutaka kufikia malengo yake
tarajiwa.
Hayo yameelezwa na Wakili Mjengi Lissu wa Kituo cha
Utawala wa Sheria na mazingira (CELG) wakati akiwasilisha mada ya vyombo vya
usimamizi wa sheri na haki za Binadamu kwa wasaidizi wa kisheria 25 kutoka
mashirika yasiyokuwa ya kiserikali Wilayani Kiteto.
“Umefika wakati baadhi ya viongozi wa Serikali wanakuwa
sio wazalendo,waadilifu katika nyazifa zao walizonazo huku wakionekana kuwasaliti
wananchi kwa kushindwa kufanya maamuzi yenye tija kwa maslahi yao binafsi”.
Alisema haya yatakwisha endapo jamii itaendelea
kuelimika na kujua wajibu wao na kuhoji na hata kukataa kile kinacholazimishwa
na watawana wao ambacho kinaaminika kuwa hakina tija na hakiwezi kuwa na
maslahi na Taifa kwa baadaye.
Alitolea mfani wa Jinsi deni la Taifa linavyozidi kukuwa
akisema kuna baadhi ya viongozi wamelewa madaraa wakisema kuaminika kwa nchi ya
Tanzania kwa wafadhili imekuwa fursa ya kuendelea kukopa bila kufikiri namna ya
kulilipa deni hilo.
Kwa upande wake Mashaka Saidi Fundi (mjumbe) alisema anashangazwa na mfumo uliopo Tanzania kuwa
watu wote wanalalamika wakiwemo viongozi vyama na Serikali na hata wasomi
badala ya kutafuta ufumbuzi wa kutatua matatizo.
“Nilimsikia Katibu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana akiwa
Dodoma analalamikia baadhi ya Viongozi wa Serikali wanaowajumu wananchi kwa
Nyanja mbalimbali akiwataka wawajibike akidai huko ni kukwepa majukumu yake
kuwa alipaswa kuchukua hatua dhidi ya
viongozi hao”.
Nae Hassani Konki akiongea kwa jazba alisema utaratibu
huu utazaa Taifa la watu wasio waadilifu wenye kupinga Serikali yao iliyopo
madarakani huku Viongozi wao wakitumia nguvu kubwa kuzuia na hata kuwaua.
Alidai katika maeneo mengi kumekuwepo na vurugu za
uchaguzi zinazojitokeza kwa kutowaamini wasimamizi kwa madai ya kulindana jambo
ambalo limeleta madhara makubwa kwa wananchi yakiwemo maafa.
Katika mafunzo hayo washiriki hao wamelaani vitendo
vunavyo jitokeza vya mauaji kati ya wakulima na wafugaji kila mara huku
Serikali ikidaiwa kushindwa kuyadhibiti kwa kile kilichodaiwa kuwepo kwa Rushwa
na ukabila.
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni