WAZIRI NAGU ABARIKI MAITI KULIPIWA MOCHWARI

     Waziri Nagu akifafanua jambo kwenye moja ya mikutano mjini Katesh Picha Na Mohamed Hamad


Waziri Nagu abariki maiti kulipiwa mochwari

NA.MOHAMED HAMAD. MANYARA
Waziri  wa nchi ofisi ya Rais na utumushi wa umma uwezeshaji na (MB) Hanang mkoani Manyara
DR. Mery Michael Nagu ameridhia tozo wanazotozwa marehemu katika
Hospitali ya Tumaini kuwa ni sahihi kutokana na uendeshaji wa mochwari


Akizungumza hayo mjini Katesh hivi karibuni katika kikao chake na
wananchi ambacho kiliibua maswali mengi yanayohusu maendeleo ya Jimbo
hilo DK Nagu alisema haoni tatizo la kutozwa fedha marehemu kwakuwa
hizo ni gharama za uendeshaji

“Ndugu zangu wananchi hata mimi nikifa itabidi mnichangie na nitazikwa
hapa hapa si ndio...ili tuwe na sehemu endelevu na yenye kujiendesha
lazima tuwe na utaratibu wa kutoza fedha za kuendeshea sioni tatizo
hapo”alisema Dk Nagu huku wananchi wakiguna

Wakati majibu hayo yakitolewa  baada ya muuliza swali kutaka majibu ya
kuridhisha wananchi hao walionekana katika hali ya kutoridhika na
kuzomea wakisema utaratibu huo haukubaliki hata kidogo kwani hiyo ni
sehemu ya huduma na sio biashara

Tatizo la migogoro ya ardhi,maji,na hatma ya kiwanda cha simenti
likatakiwa majibu yake ambapo Saidi Ally,Sabo,na marsel Msafili
walitaka ufafanuzi na majibu sahihi kutoka kwa Mbunge wao Dk Mery Nagu

Sauti za chini chini za manunguniko yalizidi kutoka kwa wananchi
yakionyesha  kutoridhika na utawala huo huku wakilaumu waziwazi mganga
mkuu wa Hospitali ya Tumaini,Idara ya ardhi na maji kuwa tatizo katika
wilaya hiyo

DK. Mery Nagu katika kila swali lililoulizwa alimwita mhusika ambapo
baada ya majibu kutolewa na kuonekana kutoridhisha wananchi
aliyaongezea kwa kusema kuwa Hajanunuliwa na kuwekwa mfukoni kama
walivyosema baadhi ya wananchi

“Ndugu zagu sijanunuliwa na wala sinunuliki kila aliyeguswa hapa
atasema mwenyewe ili mjue kuwa siwezi kununulika wala kununulika, na
mjua mbunge wenu nimefanya mambo makubwa sana acheni kusikiliza mamene
ya vijiweni”alisema Dk Nagu

Kuhusu sakata la maji alikiri kuwepo kwa adha kubwa ya maji Hanang
akisema hata Mh Rais analijua na kuna jitihada kubwa zilizofanywa na
Serikali akishirikiana nayo kuhakikisha wananchi wanaondokana na kero
ya maji

Kuhusu Viwanja walivyotozwa wananchi 20,000 bila kuvipata alisema
jitihada zinaendelea kutafutwa ukweli wa jambo hilo na mashamba saba
yaliyokuwa ya wawekezaji alidai kwa jitihada zake mawili yamerudi kwa
wananchi huku suala la kiwanda akidai hatua za mwisho zinaendelea na
kitaajiri vijana wengi

Mwisho

Maoni