CCM Kiteto yagawa wanachama
NA.MOHAMED HAMAD MANYARA
CHAMA cha mapinduzi CCM
wilayani Kiteto mkoani Manyara kimegawanyika vipande kutokana na joto la
kisiasa linaloendelea kupanda kila kukicha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015
Taarifa za uhakika ndani ya
chama hicho zimeeleza kuwa hakuna mahusiano mema ya kikazi kati ya Mjumbe wa
Halamshauri Kuu ya CCM Emmanuel Papiani na Mbunge wa Jimbo la Kiteto Benedict
Ole Nangoro ambao wote wanawania Jimbo hilo
Akizungumza na MTANZANIA
katibu wa Mbunge huyo Singo Ndoera jana alisema Mbunge Nangoro hawezi kuungana
na msafara anaofanya Mjumbe wa Halamshauri kuu ya CCM Taifa Emmanuel Papian kwa
kuwa unabagua wanachama kwenye msafara
wake
“Kiukweli pamoja na kuwa
ziara hiyo ni njema kuzungumzia katiba na uandikishaji wa daftari la wapiga
kura naweza kusema kuna ubaguzi unaofanywa na uongozi wa msafara huo kwani
baadhi ya watu hawatakiwi kuwepo”alisema Ndoera
Alisema ziara aliyomaliza
hivi karibuni baada ya hii alimfukuza mwanachama mmoja wa CCM aliyejulikana kwa
jina la Dura Msonde katika Kijiji cha Matui kwa madai kuwa Hayupo kwenye kambi
yake
Tumeamua kumwachia MNEC
amalize ziara yake na kisha nasi tutaanza ya kwetu ambapo nasi tutazunguka
wilaya yote kuongea na wananchi ambao wanahamu ya kuongea na Mbunge wao juu ya
maendeleo yao
Mjumbe huyo wa CCM Taifa katika
ziara yake ameambatana na katibu wa CCM wilaya Abeid Meila, Katibu wa mwenezi
Christopher Parmet, na mwenyekiti wa Vijana CCM wilaya Bw,Emmanue na Mkuu wa
Wilaya ya Kiteto Kanal Samweli Nzoka,
Kuhusu tuhuma za kufukuzwa
mwanachama huyo kwenye msafara wa MNEC huyo alisema hajamfukuza na wala hana
sababu ya kufanya hivyo na kwamba kazi ya chama haina ubaguzi na ndio maana
anazunguka na viongozi wa ngazi mbalimbali wa CCM katika kufikisha ujumbe wake
Ujumbe katika ziara hiyo ya
MNEC ni kuwataka wananchi kujiandaa kujiandikisha daftari la kudumu la wapiga
kura,kusoma katiba pendekezwa na kuipigia kura, na kulaani mauaji yanayoendelea
kujitokeza ya wakulima na wafugaji kila mara
Alisema changamoto anayoipata
katika ziara yake ni pamoja na kuulizwa maswali mengi kuhusu ahadi alizokwisha
kuziahidi wakati wa kumwaombea kura Mbunge huyo zikiwemo za maji,umeme na hata
mawasiliano ya simu akisema Mbunge huyo amekuwa
mzito kwenda kuongea na wananchi
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni