Jimbo la Kiteto lawaniwa na watano.
Na Mohamed hamad Manyara.
JUMLA ya watu watano wametajwa
kuwania Jimbo la Kiteto lililopo mkoani Manyara kumrithi Mbunge Benedict Ole
Nangoro (CCM) anayemaliza muda wake mwaka huu
Waliotajwa kuingia katika
kinyanganyiro hicho ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Emmanuel
Papian,Amina Saidi Mrisho (CCM) anayefanya kazi tume ya Takwimu Taifa,Jonathani
Kilani kutoka CHADEMA na Mashaka Said Fundi wa SAU
Hata hivyo wakati wananchi
hao wakijitokeza kuwania Jimbo hilo taarifa za
uhakika kutoka kwa Mbunge wa Jimbo hilo
Benedict Ole Nangoro zinaeleza kuwa anakusudia kutetea nafasi yake hiyo
“Tunahitaji wengi wajitokeze
ili tuwachuje na kumpata kiongozi bora atakayekomboa Jimbo la Kiteto ambalo kwa
sasa linachangamoto nyingi zikiwemo za migogoro ya ardhi” alisema mmoja wa
wananchi wilayani humo
Kwa miaka saba wananchi wa
Kiteto wamekuwa kwenye kipindi kigumu cha maisha kutokana na kutumia muda
mwingi kwenye migogoro ya ardhi kuliko kufanya shuhuli zinhgine za maendeleo
Akizungumza hayo Ibrahimu
Msindo (mwananchi) hivi karibuni alisema miaka saba iliyopita imekuwa shubiri
na historia kwa wanakiteto ambapo kila mmoja anachakusema baada ya wengi wao
kufanyiwa ukatili wa aina yake
“Kuna waliouawa shambani,wengine
machungajini na wengine kufungwa jela kwa madai ya kuvamia maeneo na wengine
kuteketezewa mali
zao kutokana na ghasia zilizoibuka wilayani humo”alisema Msindo
“Tunataka Kiongozi atakaye
jibu matatizo haya kati ya hao kwani mwenye mamlaka ya kumweka kiongozi madarakani
ama kutomweka ni mwananchi mwenyewe na sio vinginevyo”alisema
Hata hivyo katika hatua hiyo
wananchi wamewataka waliojitokeza kuwania Jimbo hilo
kujipima juu ya yaliyojitokeza kwa wananchi kuuana wengine kufilisika na hata
kupata vilema vya maisha kama wanatosha katika
nafazi hiyo
Toka kuzindiliwa Jimbo la
Kiteto mwaka 1974 wilaya ya Kiteto imeongozwa na wabunge watano akiwemo Abdalah
Kimosa,Erasto Losioki, Jumanne Surumbu ambaye aliongoza kwa miezi
mitatu,Benedict Kiroiya Loosurutya na Benedict Ole Nangoro aliyopo madarakani
sasa.
MWISHO
Maoni
Chapisha Maoni