Kiteto na mkakati wa kuboresha elimu.
Na Mohamed Hamad Manyara
Sekta ya elimu ni taa ya
maendeleo,nasema hivi nikimaanisha hakuna Taifa lililoendelea bila elimu, mataifa hayo yalifanikiwa kutokana na kuweka
elimu kuwa kipao mbele chao katika bajeti za maendeleo
Kwa miaka saba iliyopita
wilaya ya Kiteto na mkoa wa Manyara kwa ujumla elimu haikuwa ikipewa nafasi ya
kutosha, hivyo wanafunzi walionekana shuleni kama
moja ya eneo la kusogeza umri ili waweze kuolewa ama kuoa
Na moja ya sababu zilizotajwa
ni uhaba wa samani na thamani,waalimu kuwa wachache,mazingira duni ya
kujifunzia na kufundishia,malalamiko ya waalimu bila kutafutiwa ufumbuzi pamoja
na uhaba wa nyumba za walimu
Kutokana na changamoto hizo
kiwango cha elimu Kiteto na Manyara kwa ujumla kilishuka katika miaka hiyo siku
hadi siku huku wananchi wakiendelea kukosa haki ya msingi kupata elimu sahihi
ambayo ilipaswa kutolewa na Serikali
Wilaya ya Kiteto kwa miaka ya
2010 iliendelea kushika nafasi mwisho kati ya wilaya sita za mkoa wa Manyara
zikiwemo Babati mjini, Babati vijijini, Mbulu,Hanang, Simanjiro na Kiteto
yenyewe
Katika kukabiliana na
changamoto hizo ilisaidia wilaya ya Kiteto na mkoa kwa ujumla kupanda kielimu
jitihada kubwa zilifanywa zikiwemo zile za kuhakikisha wanapunguza malalamiko
ya waalimu pamoja na kuboresha sehemu za kujifunzia na kufundishia
Afisa elimu wa wilaya ya
Kiteto Emmanuel Mwagala katika jitihada za kukuza elimu wilayani Kiteto
alieleza kuwa wilaya imepata mafanikio makubwa yakiwemo kutoka katika nafasi ya
mwisho hadi ya pili kimkoa
Alisema kwa sasa Kiteto
inashikilia nafasi ya pili kimkoa kwa miaka miwili mfululizo kutokana na
mikakati mbalimbali ikiwemo ya wanafunzi kula shuleni tofauti na hapo awali
walipokuwa wanalazimika kushinda na njaa wakiwa shule hadi watakaporudi
nyumbani
Mwingine ni waliongeza idadi
ya waalimu ambapo awali shule moja ilikuwa na mwalimu mmoja ama wawili huku
ikiwa na idadi ya wanafunzi zaidi ya mia tano kutokana na Serikali kushindwa
kuajiri kulingana na uhitaji wa waalimu katika shule nyingi hapa nchini
Motisha nayo ilisaidia kwa
kiwango kikubwa kwa waalimu na hata wanafunzi waliokuwa wanafanya vizuri ambapo
walileta ushindani wa hali ya juu jambo lililofanya kiwango hicho cha elimu
kupanda alisema Mwagala
Hata hivyo Afisa huyo wa
elimu katika mahojiano maalumu alisema jumla ya wanafunzi bora 17 wakiume 9 na wakike 8 kati ya 20 waliofanya
vizuri mkoani Manyara walitoka Kiteto
“Niseme tu hata mwanafunzi
bora kimkoa wametoka wilaya ya Kiteto tena katika shule ya msingi Boma, huku
shule tatu za kiteto zikiendelea kuchuana ikiwemo ya Boma, Lalakir, na Namelock”alisema
Mwagala
Alisema kuwa mkoa ulihamasika
nao na kupongeza wilaya ambapo walitoa kikombe cha dhahabu huku Taifa nao
wakihamasika na kutoa medani moja ya dhahabu pamoja na ya fedha moja
Shule mbili zilipewa mil 3
kila moja kwa jitihada kubwa za katika kuchupa kutoka nafasi za nyuma hadi
kuingia katika alama zuri ambapo shule hizo ni partimbo na ilera na kwamba zilifanikiwa
kupata kiasi cha mil 3 kila moja kama moja ya
motisha
Kuhusu changamoto za uhaba wa
nyumba za waalimu madarasa mapunjo ya waalimu
pamoja na samani na thamani Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya
Bosco Ndunguru aliyema Serikali imejipanga kukabiliana na tatizo hilo
Alisema suala la madawati
kuna fursa Kiteto ya kuwa na msitu wa Suledo ambao umeanza kuvunwa mbao
utatumika kama fursa ya kuhakikisha kila shule
inapata madawati ya kutosha ili kupunguza adha ya wanafunzi kukaa chini
Kwa upande wao wadau wa
maendeleo wamekosoa jitihada zinazofanywa na wilaya kuendeleza jitihada hizo
wakisema bado kuna malalamiko ya waalimu ambayo hayakashuhulikiwa ipasavyo
hivyo kuna uwezekana wa kushuka tena elimu
“Ninachojua bado hadi leo
waalimu wanatishiwa amani mahali pa kazi na baadhi ya wananchi wa misingi ya
kufuatilia wanafunzi watoro Serikali haijajipanga sawasawa kwani ni
hatari”alisema Abasi Famao mdau wa elimu
Kwa upande wa chama cha
waalimu wilayani Kiteto wamedai iko haja ya kuwepo kwa mfumo mzuri wa
kushuhulikia matatizo ya waalimu Serikalini tofauti na ilivyo sasa kuwa kada ya
waalimu inaonekana kama haina umuhimu ndani ya
jamii
Utakuna mwalimu anakamatwa
akifundisha eti kwasababu tu hajalipa mchango wa maabara, hivi hakuna njia
nyingine mbadala ya kupata fedha hiyo mpaka umkamate mwalimu wakati akifundisha
alihoji Ghambos Sule mwenyekiti wa chama cha walaalimu mkoani Manyara
INAENDELEA…
Maoni
Chapisha Maoni