Mashirika ya umma lawamani
Kiteto
NA.MOHAMED HAMAD MANYARA
Mashirika ya umma wilayani
kiteto mkoani Manyara yanayojihusisha na masuala ya matumizi bora ya ardhi
pamoja na haki za binadamu yametupiwa lawama kwa kushindwa kuingilia kati
migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji inayoendelea kurindima kila
kukicha
Wakizungumza hayo wananchi wa
mji wa Kibaya jana walisema hawaoni uwepo wa mshirika yanayojihusisha na
matumizi bora ya ardhi na hata yale ya haki za binadamu kutokana na wakulima
kuendelea kujeruhiwa na wafugaji kwa madai kuwa wanaharibu mazingira
Kwa sasa mashirika hayo ya
umma yanayotajwa kuwa lawamani ni pamoja na shirika la KINNAPA,CORDS, NAADURARO
na SWEAT, yanayofanya kazi wilayani kiteto ya matumizi bora ya ardhi
Mengine ni KIWOCOA,WASHEHABIKI,
ambayo yanafanya kazi ya utetezi wa haki za binadamu kuwa kwa pamoja
yameshindwa kuwa msaada katika sakata la wakulima na wafugaji wilayani hapo
wanaohasimiana na hata kuuana
Kwakizungumxa juu ya sakata
hili baadhi ya viongozi wa mashirika hayo kiwemo Joseph Kaaya wa shirika la
WASHEHABIKI alisema kazi hiyo haina tija tena kwao baada ya kuundwa tume ya
Waziri Mkuu Pinda kuchunguza mauaji hayoi
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni