Migogoro ya ardhi Kiteto itamalizwa na viongozi wa
dini
NA.MOHAMED HAMAD MANYARA.
Serikali imeshauriwa kuacha
kutumia Jeshi la Polisi kushuhulikia migogoro ya ardhi kati ya wakulima na
wafugaji Kiteto badala yake iwatumie viongozi wa dini ambao watatumia vitabu
vitakatifu kurejesha amani inayoendelea kutoweka.
Kauli hiyo imetolewa na
Mch.Richard Mwenda wa kanisa la Full Gospal Bible Felloship Kiteto mwishoni mwa
wiki wakati akizungumzia njia ya kurejesha amani na athari wanazopata viongozi
wa dini yanapojitokeza mauaji wilayani humo
“Hatuna amani viongozi wa
dini tunapoitwa mara kwa mara kuzika watu wanaouawa tena kikatili kwa silaha za
jadi,kuchinjana na hata kupigana risasi kutokana na migogoro ya ardhi mbona
hapo mwanzo hatukuwa hivi?”alihoji Mch Mwenda
Alisema kazi ya viongozi wa
dini ni kujenga watu kiimani ili wawe na hofu ya Mungu na mauaji ni matokeo ya
watu kuwa na rogo ngumu iliyosababishwa na mfumo mbovu wa baadhi ya viongozi
kuingia madarakani kwa kutumia ukabila
Kamati ya Waziri Mkuu Mizengo
Pinda iliyopo Kiteto inafanya kazi nzuri kuwarejesha watu katika misingi ya
imani dhidi ya wenzao ambayo ilitoweka baada ya kugombanishwa na baadhi ya
viongozi wasiowaadilifu kwa misingi ya kisiasa na ukabila
Kutumia Jeshi kukabiliana na
wauaji ambao nao wanasilaha kamwe hawataweza kufanikiwa kamati ya Pinda iungwe
mkoni na dini na Serikali ifanikishe
zoezi hilo na
sio kutumia Jeshi la Polisi ambalo limesababisha madhara makubwa kwa wananchi
Awali Serikali ya Kiteto
ilitumia Jeshi la Polisi katika kukabiliana na wakulima waliopo katika maeneo
ya Emboley Murtangos kuwatoa kwa nguvu na hata kuteketeza mali zao kwa madai ya kuharibu
mazingira
Kurejesha amani ni gharama na
ni rahisi kuvunjika, Serikali ya Kiteto ilifanya kosa kutumika kama wakala wa
jamii ya kifugaji wamasai kuwafukuza wakulima kwa gharama za wafugaji kuchanga mifugo
yao jambo
ambalo Waziri Mkuu alilikemea akidai ndicho chanzo cha migogoro hiyo
Akiwa katika mwendelezo wa
mikutano na wananchi Mwenyekiti wa kamati ya maridhiano ya wakulima na wafugaji
Askofu Amos Joseph Mhagachi alisema hatua iliyofikiewa inaleta matumanini ya
kurejea amani Kiteto hasa wananchi wanapoendelea kutoa ushirikiano
“Tunaendelea kukutana na
makundi mbalimbali ya wananchi wanatupa ushirikiano mzuri wa kuongea ukweli
tena ukweli mtupu ambao hata sisi tunauona, sasa kamati hii sio mahakama
tutaandika taarifa kisha kuiwasilisha kwa mwenyewe Waziri Mkuu”
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni