Mjamzito wa miezi 9 afariki kwa kugongwa na Bodaboda
Kiteto
NA. Mohamed Hamad Manyara
Mwanamke mmoja mkazi wa eneo
la Jangwani kata ya Bwagamoyo wilaya ya Kiteto mkoani Manyara amepoteza maisha
baada ya kogongwa na pikipiki maarufu bodaboda wakati akitokea kliniki ya
Hospitali ya Kiteto akielekea nyumbani kwake
Muda mfupi baada ya kufariki mwanamke
huyo kwa zaidi ya saa moja mtoto amedaiwa kuendelea kucheza tumboni na baadaye
alitulia wakati jitihada za kutaka kumpasua zikiendelea, ndugu walikataa asifanyiwe upasuaji huo
Hata hivyo taarifa kutoka
Hopitalini zinaeleza kuwa mwanamke huyo ambaye jina lake halikufahamika
mapema alivunjika mguu na mkono huku dereva huyo naye akidaiwa kuwa hoi na amelazwa
hospitali ya wilaya ya kiteto akijiuguza majeraha aliyoyapata baada ya
kuburuzika
“Ndugu wa marehemu wamekataa
asifanyiwe upasuaji baada ya vipimo kuwa mtoto naye amefariki hivyo wamemchukua
kwaajili ya maziko ambayo yamefanyika saa saba mchana huu katika makaburi ya
Jangwani”alisema mmoja wa watumishi wa Hospitali hiyo
“Ajali ilitokea jana saa tano
za asubuhi muda mfupi baada ya mwanamke huyo kutoka kliniki na alipofika eneo
la darajani njia ya kuelekea Handeni akagongwa na kijana aliyefahamika kwa jina
la Kurwa Ramadhani (18) ambaye amelazwa hapa aliyekuwa akiendesha pikipiki
maarufu bodaboda”kilisema chanzo cha habari
Kwakweli pikipiki
zinakimbizwa sana
barabarani na sio huyo tu aliyegongwa leo kuna mtoto mmoja wa Ibrahimu Elisha
naye muda mfupi hapa kagongwa kavunjika mguu kaletwa hapa kwaajili ya matibabu kilizidi
kueleza chanzo hicho
Kwa mujibu wa ndugu wa
marehemu huyo ambao hawakutaka kutajwa majina yao
na ambao hawakutaka kuweka wazi juu ya suala hilo walisema wameamua kuuzika mwili huo
ukiwa haujafanyiwa upasuaji wa kutoa kiumbe hicho cha miezi tisa tumboni
ambacho nachi kimedaiwa kupoteza uhai
Baadhi ya wananchi
waliozungumzia tukio hili akiwemo Ramadhani Issa alisema kilichofanywa na ndugu
hao sio chakiungwana kwani walipaswa kukubali apasuliwe ili waone kama mtoto huyo yu hai ama amefariki na sio kuuzika mwili
huo ukiwa hivyo
Jeshi la Polisi wilayani
kiteto limekiri kutokea tukio hilo
na kudai linaendelea kumshikilia kijana huyo aliyesababisha kifo cha mwanamke
huyo na kwamba walidai chanzo cha ajali ni mwendokasi uliosababisha kushindwa
kumudu pikipiki
mwisho
Maoni
Chapisha Maoni