MNEC Kiteto ahamasisha wananchi kusoma katiba
NA.MOHAMED HAMAD MANYARA
Mjumbe wa Halamshauri kuu ya
CCM Taifa Emmanuel Papiani amewataka wananchi wilayani Kiteto mkoani Manyara kusoma
kwa makini rasimu ya katiba pendekezwa kwa lengo la kuja kuipigia kura
Wilayani ya Kiteto imepata
nakala 6900 ambazo zimegawanywa kwa makundi tofauti yakiwemo ya wananchi na
taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za Serikali kwa lengo la kusomwa
Akizungumza jana kwenye
mfululizo wa mikutano aliyoanza vijijini mjumbe huyo alisema ameamriwa kuitish
vikao hivyo kwa lengo la kuhakikisha wananchi wanasoma rasimu hiyo pamoja na
kujiandaa kwa zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura
“Rasimu pendekezwa ya katiba iligawanywa
kata 19 zilizopo wilayani Kiteto na kwa taasisi za elimu, mashirika yasiyo ya
kiserikali,taasisi za kidini na kwenye
maeneo ya mikusanyiko ya watu, someni muelewe kilichomo kisha mfanye
maamuzi sahihi ya kuisaidia nchi”
Pia aliwataka wananchi hao
kujiandaa kupokea daftari la kudumu la wapiga kura ambalo litaanza kwa wananchi
kujiandikisha Mkoani Manyara baada ya mikoa mingine kumaliza
Baada ya kumalizika kwa
hutuba hiyo wananchi wakapata fursa kutaka ufafanuzi wa kiongozi huyo juu ya
mauaji yanayoendelea kujitokeza kuwa nini kauli ya chama baada ya kukaa kimya
kwa muda mrefu bila kusikia tamko lao
Awali akiuliza swali Neema
Kivugo (mwananchi) kwa niaba ya akinamama alitaka kauli ya chama juu ya mauaji
yanayoendelea hasa kwa wanawake na watoto kutokana na migogoro ya ardhi
iliyodumu kwa miaka sita mfululizo
“Mhe Mjumbe wa Halmashauri
kuu ya CCM Taifa nini kauli yao
juu ya kinachotokea Kiteto kwa akinamama na watoto wanaouawa kutokana na
migogoro ya ardhi ambayo kwa sasa chama kimeendelea kuwa kimya”
Kwa upande wake Jastine
Lukumay aliuliza lini chama kitachukua hatua ya kuzuia umwagikaji wa damu za
watu wasio na hatia ili hali wanaoua wanafahamika huku Serikali ikiwa kimya?
Akijibu maswali hayo Mjumbe huyo
wa Halamshauri Kuu ya CCM Taifa aliwataka wananchi hao kulaani mauaji hayo
ambayo Taifa limesikia kilio chao na kuunda tume nyingi zilizofika kuchunguza
na kuandika ripoti zao kisha kupeleka kwa uongozi wa ngazi ya juu
Christoph Parmet katibu
mwenyezi wa CCM Taifa akitoa ufafanuzi kwa niaba ya chama alisema CCM
haitasubiri wapinzani kuja kuwachambua juu ya kilichotokea bali wananchi
wafanye maamuzi magumu ya kuwakataa viongozi wasiokuwa waadilifu
“Nilimshauri Mbunge wangu Benedict
Ole Nangoro (CCM) katika vikao mbalimbali vya chama ajitokeze kwa wananchi kuonyesha
hisia zake juu ya mauaji hayo akashindwa, kila mahali analalamikiwa naagiza
marafiki zake waende kumwambi asipolaani mauaji hayo asije kusimama kwenye
mikutano milele kupitia CCM kuomba kura”alisisitiza huku akipigiwa makofi mengi
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni