RC Manyara aunda tume kuchunguza migodi 16 iliyoungua.
NA. MOHAMED HAMAD MANYARA
Mkuu wa mkoa wa Manyara Dr Joel
Bendera ameunda tume ya kuchunguza chanzo cha moto uliotokea hivi karibuni
katika migodi 16 ya Tanzanite kitalu B (Opec) iliyopo Mererani wilayani
Simanjiro.
Moto uliunguza migodi ya
wachimbaji wadogo machi 8 saa 10 jioni
na kusababisha hasara inayokadiriwa kuwa ya sh 2.4 bilion ambapo hata hivyo
haukuleta madhata kwa watu kupoteza maisha
Akizungumza hayo mkuu huyo wa
mkoa alisema wataalamu hao wamebobea katika Nyanja mbalimbali na kwamba
watafanya kazi kwa uadilifu mkubwa ili kuweza kutoa majibu mazuri
yatakayofanyiwa kazi na Serikali
“Nimeamua kuunda tume ili
kuondoa manung’uniko ya wananchi juu ya kilichotokea kwani hakuna anayeonekana
kusema jambo likakubalika bila kuleta utaalamu ambao utatusaidia Serikali na
wananchi”alisema Bendera
Kwa upande wake Zacharia
Lukas diwani wa kata ta Endiamtu alisema hatua hiyo itaondoa utata ambao umegubikwa
baada ya kutokea tukio hilo
ambalo wachimbani wadogo wameathirika
Hivi sasa baadhi ya wamiliki
wa migodi hiyo wameathirika kwa kiasi kikubwa kwani moto uliteketeza kila kitu
katika maeneo hayo ya migodi hiyo ambazo zilisaidia katika uchimbaji wa madini
ya Tanzanite
Kwa upande wa wanachi
waliozungumzia juu ya hatua hiyo walipongeza hatua hiyo wakisema ni mwafaka kwa
sasa ambapo utata ulijitokeza juu ya chanzo cha moto huo ambao Tanesco waliruka
kimanga kuwa hawakusababisha wao
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni