Wakulima 9 Kiteto wanusurika kuuawa,walazwa
·
Kamati ya Pinda
yaenda kuwapa pole
Na. Mohamed Hamad Kiteto
Jumla ya wakulima 9 wa kijiji
cha Kimana kata ya Partimbo wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto
baada ya kukatwakatwa mapanga pamoja na kuchomwa mikuki wakiwa shambani na
jamii ya kifugaji wamasai
Tukio hilo limetokea march 31 mwaka huu katika
maeneo tofauti ya kata ya Partimbo ambako jamii ya kifugaji wamasai wamedaiwa
kuendeleza ukaidi wa agizo la Serikali la kujichukulia sheria mkononi kuvamia wakulima shmbani na
kuwapiga
Waliojeruhiwa ni pamoja na
Hamidu majidi (42) wa eneo la katikati Jaki Mgomba (32) wa eneo la Kisima, Sefu
Frenki (33) wa eneo la kisima, na mmoja aliyefahamika kwa jina moja la
Ramadhani ambaye alijeruhiwa sehemu za kichwani
Wengine ni Kizota Saitoti
(35),Paulo Disulile (39) wa kisima aliyevunjwa mkono, Yahaya Mussa (33)
aliyejeruhiwa kichwani na kuvunjwa kidole cha mkono,Mbaya Malogo (42) na mmoja
ambaye alijulikana kwa jina moja la Yusuph
“Tunachoshangaa toka tumepata
matatizo haya hakuna kiongozi yoyote wa Serikali ya Kiteto aliyefika japo
kutupa japo pole kwa tunayofanyiwa na hawa wenzetu wamasai hatujui
wanafurahishwa ama vipi”alisema Jaki Mgonda majeruhi aliyechomwa mkuki kiunoni
Alisema kutofika kwa viongozi
hao wa wilaya ni picha tosha kwa umma kuwa kuna jambo lililojificha akidai kama kuna mahali pa kuanzia kufuatilia kujua ukweli wa
sakata hili ni kuanzia hapo kwani hakuna sababu zozote za msingi wao kutofika
wakati ofisi zao ziko karibu na Hospitali ya wilaya na ndipo wanapopita kwenda
mahofisini
Alienda mbali zaidi akisema kama tume iliyoundwa na Waziri Mkuu kwaajili ya kutafuta
ufumbuzi wa migogoro hiyo walifika hospitalini na kutoa pole wao walipata
uchungu gani na kwanini viongozi wa eneo husika
huwa hawafiki alihoji
Viongozi wa wilaya
waliotarajiwa kufika ni pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kiteto Benedict Ole
Nangoro pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Kimiang’ombe Nzoka na wengine ambapo baada ya kutafutwa
kwa njia ya simu juu ya lalamiko hilo hawakupatikana
“Inaumiza sana kuona viongozi
wetu wa wilaya wanaonekama kuwa mstariu wa mbele kubagua watu kwa kutoshirikiana
nasi mpaka tume ya Waziri Mkuu iguswa na
kufika ili hali siku zote wapo na wanaonekana mitaani na magari yao alisema
ambapo alidai walichomwa mikuki,
Kukatwakatwa mapanga pamoja
na kushambuliwa kwa fimbo sehemu mbalimbali za miili yao”alisema kwa uchungu mhanga Jaki aliyekuwa
na jeraha la mkuki kiunoni akidai ubaguzi ni mkubwa
Kwa mujibu wa taarifa za
uhakika kutoka ndani ya kamati ya Pinda iliyopo Kiteto zilisema baada ya
kusikia tukio hilo mara moja walifika na
kushuhudia majeruhi hao ambao wengi wao walikuwa na mjeraha mbalimbali ya miili
yao wakiwemo
wale waliochomwa mikuki na mwingine kuvunjwa mkono
“Tulifanya mahojiano na
wahanga kwakweli vitendo hivi ni vibaya sana
kuna haja gani wewe mfugaji kuingiza mifugo yako shambani kwa nguvu halafu
unampiga mkulima haya mamlaka umepata wapi wakati nchi hii inaongozwa kwa
sheria”alisema mmoja wa wanakamati hiyo
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni