Compassion wasaidia watoto 1243 Kiteto
NA. MOHAMED HAMAD MANYARA.
JUMLA ya wanafunzi 1243 ambao
wazazi wao hawana uwezo wilayani Kiteto mkoani Manyara, wamepata ufadhili wa
kusomeshwa na Compassion Interanation Tanzania kwa miaka 22 hapa nchini
Akizungumza siku ya mtoto wa
Afrika mchungaji Dominick Chilambo wa kanisa la Anglikan KCC Kibaya alisema
nafasi hiyo ni adimu kwa watoto hao ambao wengi wao wamekosa nafasi hizo kwa
wazazi wao kutokuwa na uwezo wa kuwasomesha
“Najua nafasi hii ni adimu
kuna watoto wenzenu wamebaki nyumbani hawaendi shule, ni kutokana na sababu
mbalimbali zikiwemo wazazi kushindwa kumudu gharama za masomo, na hata wengine
kupata mimba nyinyi mmebahatika tumieni nafasi hii kupata elimu”alisema
Mch.Chilambo
Alisema pamoja na wadau kujitokeza
kuwasaidia mtoto kupata elimu kwa sasa wanakabiliana na changamoto nyingi
zikiwemo mwamko mdogo wa wazazi kwa kuwatumia watoto wao kama
vyanzo vya mapato kwa kuwaoza kwa wanaume
Alitaja sheria ya ndoa ya
mwaka 1971 ambayo mzazi ana ridhaa kuozesha mwanae kwa mamlaka aliyonayo
akisema, wengi wao wameolewa na wengine kupata ujauzito na kuacha shule kwa
kukosa usimamizi makini wa wazazi na walezi wako
“Bado Serikali haijawa makini
katika kuunda sheria ya motto, kwani mpaka sasa kuna sheria inasema motto ni
yule mwenye umri wa chini ya miaka 18 lakini leo Taifa linashuhudia ndoa za utotoni
watoto wa kike wakiozwa chini ya umri wa miaka 18”alisema
Kwa upande wake Joseph Kaaya
mwangalizi wa haki za binadamu katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika
alisema, kuwa imekosekana dhamira ya dhati kwa Serikali ya kumlinda mtoto ndidi
ya maadui ambao hawapendi ajiendeleze kielimu
Hata sisi wanasheria tumekuwa
hatuelewi cha kufanya kwani utamkamata mhalifu ambaye amesababisha mtoto kuacha
shule na kumpeleka mahakamani lakini anakuja mzazi anasema nimemwozesha kwa
ridhaa yake na sheria inamtambua alisema Kaaya
Nao wanafunzi katika risala yao mbele ya mgeni rasmi waliomba wadau mbalimbali wa
elimu kuingilia kati kuhusu hujuma hizo kwa kushinikiza wabunge kubadilisha
sheria kandamizi ikiwemo ya ndoa ambayo walisema kama
hali hii haitakomeshwa miaka mitano ijayo watoto wa kike hawatakuwa na fursa kupata
elimu
Jackson Abel Mkurugenzi wa
kituo cha kanisa la TAG cha 127 akizungumzia fursa ya elimu inayotolewa na
Compassion Internation Tanzania alisema kuwa mwanafunzi aliyyepokelewa ana
nafasi ya kusomeshwa kwa miaka 22
mfululizo na wafadhili pale ambapo atafuata masharti yao
Alitaja fursa kwa wanafunzi
hao kuwa ni pamoja na kupatiwa mahitaji mbalimbali na wafadhili hao yakiwemo
ada za shule,nguo,madaftari vitabu na hata kujengewa nyumba kwa wale wazazi wao
wasiojiweza ili wajimudu kimaisha
Akifafanua zaidi Mkurugenzi
huyo alisema kuwa katika misaada hiyo kwa wanafunzi hao jumla ya Tsh 120 mil
zimetumika kugharamia elimu na mahitaji ya shule kwa watoto hao
Zingine ni 10 mil zilitumika
kwa masuala ya afya za watoto hao,20 mil zilitumika kuboresha makazi na hata
kuwajengea nyumba baadhi ya watoto,na 30 mil zilitumika kugharimia mahitaji ya mtoto
mmoja mmoja katika maeneo mbalimbali ya shuleni
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni