Ng’ombe 700 kutaifisha na Serikali Kiteto
·
Wamiliki wadaiwa
kuua na kujeruhi
·
Wananchi wapongea
kamati ya ulinzi na usalama
NA.MOHAMED HAMAD
JUMLA ya ngombe 700 mbuzi na kondoo wapatao 290 wanakusudiwa
kutaifishwa na Serikali wilayani Kiteto mkoani Manyara baada ya wamiliki wa
mifugo hiyo kutokomea kusiko julikana kwa hofu ya kufunguliwa kesi ya mauaji
yaliyomhusisha mkulima mmoja na kujeruhiwa wengine wane.
Mifugo hiyo iko chini ya
ulinzi wa Jeshi la Polisi imehifadhiwa uwanja wa mpira wa miguu Kiteto kwa siku
tatu mfululizo kusubiri wenyewe kujitokeza bila mafanikio na kwamba jitihada za
kuinusuri ni kuitaifisha na kuipeleka ranchi
ya Taifa ili iweze kuhudumiwa
Waliolazwa ni pamoja na
Dominic Meena (48) ,Daudi Eraston (22) Selemani Chizenga (33) na mmoja ambaye
jinalake halijafahamika kwa pamoja walipata majeraha vichwani pamoja na kuvunjwa mikoni na vidole
“Tatizo linalojitokeza hapa kuna
baadhi ya viongozi ambao wanashindwa kutambua nafasi zao ndani ya jamii, ona
hapa kuna madiwani wanaotokana na jamii ya kifugaji wanafika eneo la tukio na
huenda wanaifahamu mifugo hiyo lakini wanashindwa kutoa ushirikiano pamoja
mifugo hiyo kuwa na alama za wamiliki”
“Kwa sasa kama hawatajitokeza
mpaka kesho tutashauriana kuona namna ya kuokoa mifugo hiyo kwa kuitaifisha na
kuipeleka ranchi
ya Taifa ili ziweze kuendelea kuhudumiwa na Serikali mpaka hapo mmiliki atakapo
jitokeza”alisema George Katabazi OCD Kiteto
Baadhi ya madiwani waliofika kushuhudia
mifugo hiyo uwanjani ni pamoja na Sekemi Sakana diwani wa kata ya Partimbo
ambako mauaji yamefanyika na Yohana Bakar diwani kata ya Namelock ambazo ni
kata za jamii ya kifugaji (maasai)
Kwa mujibu wa Mkuu wa wilaya
ya Kiteto Kanali Samuel Nzoka aliambia Jambo Leo kuwa kitendo cha jamii ya
kifugaji wamasai kususia Serikali mifugo yao ni kosa ambalo halivumiliki na sio
utetezi kwa wakosaji na kuwataka wajitokeze ili kuchukua mifugo yao na sheria
ifuate mkondo wake
Alisema mifugo hiyo inahitaji
kuhudumiwa kwa kupelekwa malishoni na hata maji hivyo toka ikamatwe haijapata
huduma hizo na kwamba madhara yanaweza kujitokeza kama itaendelea kubaki katika
eneo hilo
yakiwemo vifo
Kwa upande wake Bakari
Maunganya mwenyekiti wa wakulima
wilayani Kiteto amelaani mauaji hayo na kuishukuru kamati ya ulinzi na
usalama kuwa imekuwa msaada mkubwa katika kukabiliana na uhalifu huo
Alisema kila mara wafugaji
wameendelea kutenda uhalifu kwa kuwaonea wakulima wanapokuwa shambani kupigwa
na hata kuuawa lakini hawajawahi kutiwa hatiani kwa tuhuma hizo huku mauaji
yakiendelea
“Kwa sasa watu 41 wamepoteza
maisha kutokana kuvamiwa wakiwa shambani na jamii ya wafugaji wamasai huku
uongozi wa Wilaya ukikiri jamii hiyo kuwa tishio kwa kufanya uhalifu mara kwa
mara”alisema Maunganya
Kwa mujibu Kamanda wa Polisi
wa mkoa wa Manyara Kamishna msaidizi Christopher Fuime amekiri kutokea tukio hilo na kudai kuwa jumla
ya watu wawili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi na mara uchunguzi
utakapokamilika watafikishwa mahakamani
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni