Afisa maendeleo ya jamii ajitosa Ubunge Kiteto.
NA. MOHAMED HAMAD.
Afisa maendeleo ya jamii
wilaya ya Kiteto mkoani manyara Joseph Mwaleba, amejitosa kugombea Jimbo la
Kiteto kupitia chama cha Mapinduzi CCM lililokuwa linaongozwa na Benedict Ole
Nangoro
Nitahakikisha naduisha amani
iliyokwisha kutoweka kwa miaka zaidi ya saba huku viongozi wakishindwa
kuunganisha jamii ya wafugaji na wakulima ambao kila mara huuana
Akieleza hayo kwenye viwanja
vya CCM wilayani humo mwishoni mwa wiki aliporejesha fomu hiyo Mwaleba alisema
Kiteto ina matatizo makubwa ambayo hadi sasa hakuna kiongozi aliyefanikiwa kuyatatua
“Kwa muda mwingi niliokaa
hapa Kiteto kama mtumishi wa Serikali,Afisa
Maendeleo ya Wilaya sijaona kilichofanyika kuhusu amani ya Kiteto na badala
yake kila kukicha wananchi wameendelea kufa wakigombea ardhi”alisema Mwaleba
Katika maelezo yake hayo
Mwaleba alisema njia atakayotumia kukabiliana na tatizo hilo
ni kuwakutanisha wakulima na wafugaji ili waweze kuzungumza matatizo yao hayo na kuridhiana
Alitaja kipao mbele chake
kingine ni kuimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja ili kuondokana na umaskini
uliokithiri kwa miaka mingi kwa kutumia elimu ya ujasiria mali
Mbali na ofisa huyo wengine
waliochukua fomu ni Hajjat Amina Said Mrisho,Benedict Ole Nangoro anaye tetea
Jimbo hilo,Emmanuel
Papian na Ally Juma Lugendo
Baadhi ya wananchi
waliozungumza na Jambo leo walielezea kuwa Jimbo la Kiteto linahitaji mtu
makini, mwenye nguvu ya ushawishi, anayekubalika kwa jamii zote za wakulima na
wafugaji
Kwa kipindi chote hicho
wananchi hao wameshindwa kufanya shuhuli za maendeleo na kuishi kwa wasiwasi
kuhofia kuuawa huku umaskini ukizidi kushika hatamu na kushindwa kuchangia
maendeleo yao
MWISHO
Maoni
Chapisha Maoni