Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kiteto Bosco Ndunguru akifafanua jambo kuhusu BVR Kiteto kushoto ni Mainge Lemalali mwenyekiti wa Halmashauri.
BVR Kiteto yafanikiwa kwa 75.3%
NA.MOHAMED HAMAD
ZOEZI la uandikishaji
wananchi katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa njia ya BVR awamu ya
kwanza kati ya awamu nne wilayani Kiteto mkoani Manyara limefanikiwa kwa 75.3%.
Awamu ya kwanza imehusisha kata
za mashariki mwa wilaya ya Kiteto ambako ni kata za Kijungu,Loolera,Lengatei na
Sunya ambapo jumla ya watu 17743 wameandikishwa
“Akizungumza na Jambo leo
Bosco Ndunguru afisa mwandikishaji wa wilaya na Mkurugenzi Mtendaji alisema
zoezi hilo
limefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika maeneo hayo tofauti na ilivyotegemewa”
Alisema zoezi lilianza juni
16 mwaka huu, kata ya Kijungu imeandikisha watu 2907 sawa na 87.27% kati ya
3331,huku Lengatei ikiandikisha watu 4718 sawa na 80% kati ya watu 5842
waliokusudiwa kuandikishwa
Kata ya Loolera jumla ya watu
2235 sawa na 77.3% wameandikishwa kati
ya watu 2889 waliokusudiwa kuandikishwa huku kata ya Sunya ikifanikiwa
kuandikisha watu 7883 sawa na 68.64% kati ya 11483 waliokusudiwa kuandikishwa
Kwa mujibu wa Ofisa mwandikishaji
wa wilaya alitaja changamoto zinazokabili zoezi hilo kuwa ni pamoja na watu kutojitokeza kwa
wingi akisema jitihada zinafanyika kwa kutumia gari la matangazo kuhamasisha watu
kujiandikisha
Kuhusu mashine za BVR alisema
jumla ya mashine tano ziiliharibika na kwamba zinaendelea kushuhulikiwa na
mafundi huku zingine zikitarajiwa kuingia kwaajili ya zoezi hilo
“Kuna mashine tano
zinafanyiwa marekebisho baada ya kusumbua, wapo mafundi wanaoendelea nazo
niwaahidi tu wananchi kuwa wote wataandikishwa katika daftari hili la kudumu”alisema
Ndunguru
Kwa upande wake Ally Mzigo
mwenyekiti wa Kijiji cha Sunya (CHADEMA) alisema kituo cha Fachande kilichopo ofisi ya Kijiji
kimesimama kuandikisha na hakuna maelezo yoyote kutoka kwa waandikishaji
Kwa mujibu wa Ofisa uandikishaji
wa wilaya alikiri na kudai kuwa tatizo hilo
akidai limetokana na kukosekana kwa wino
ambao umeagizwa mkoani Manyara na mara baada ya kufika zoezi litaendelea
Kwa upande wa wananchi
waliozungumzia zoezi hilo
wamedai tatizo lililopo ni kukaa muda mrefu vituoni hali inayofanya wakate
tamaa na kurejea nyumbani kwaajili ya kutafuta riziki
MWISHO

Maoni
Chapisha Maoni