MKUTANO WA KAMPENI ZA CCM KITETO WALINDWA KWA MITUTU

Ulinzi mkali mikutano ya Ubunge CCM Kiteto

-Polisi watanda na silaha kali za moto

Na. Mohamed Hamad Manyara
JESHI la Polisi Wilayani Kiteto mkoani Manyara limelazimika kulinda
mkutano wa kampeni za Ubunge CCM chini ya ulinzi mkali, kumnusuru
mgombea Benedict Ole Nangoro mmoja wa wagombea hao asidhuriwa na
baadhi ya wanachama kwa madai kuwa, amekuwa chanzo cha migogoro ya
ardhi kati ya wakulima na wafugaji

Akizungumza hayo Abeid Maila katibu wa CCM Wilaya ya Kiteto mara baada
ya kumalizika mkutano wa kampeni kata ya matui alisema, alilazimika
kuweka ulinzi huo mkali kutokana na hofu ya kujitokeza vurugu katika
eneo hilo ambalo linachangamoto kubwa ya kisiasa

"Taarifa za kiintelejensia zilieleza kuwa Ole Nangoro alipaniwa na
wanachama hao kupigwa mawe, hali iliyosababisha niweke ulinzo mkali
ambao umewezesha kumalizika kwa mkutano huu salama salmini"alisema
Katibu huyo

"Pamoja na zomea zomea tulizoziona katika maeneo mengine tulipopita
dhidi ya Ole Nangoro, hapa tungekuwa fujo zaidi na ndio maana tukaamua
kuwaalika wenzetu wa Jeshi la Polisi waweze kutusaidia"alisema Maila

Pamoja na ulinzi huo mkali wanachama hao wa CCM waliweza kuonyesha
hisia zao kwa mbunge huyo aliyemaliza muda wake kwa kumuuliza maswali
mengi yanayofanana kuhusu migogoro ya ardhi iliyosababisha watu kuuana
na wengine kujeruhiwa

Makoyo Msukuma (mwananchi) aliuliza maswali mgombea Benedict Ole
Nangoro akisema Kata ya matui ni miongoni mwa maeneo yalioathirika na
migogoro ya ardhi na kusababisha mauaji ya wakulima na wafugaji,
alikuwa wapi kushiriki mazishi ama hata kutoa pole kwa wafiwa leo hii
anajitokeza amesukumwa na kitu gani kikubwa kulika kilichojitokeza

Swali hilo liliibua hisia za wananchi hao ambao wengine walianza
kuzomea huku polisi wakirandaranda kutaka kukabiliana na hali hiyo
kisha kupatiwa majibu na mgombea huyo kuwa alikuwa na kazi maalumu za
kiserikali nje ya kiteto zilizomfanya asiweze kufika

"Sio hapa Matui tu sijafika...ni maeneo mengi nafahamu wapo
watangulizi wangu walifika zikiwemo mamlaka husika Polisi kukabiliana
na uhalifu huo sikuona sababu ya kufika kwa wakati huo kwani wenye
mamlaka walikwisha kufika"alisema Nangoro na kuongeza

"Mgogoro wa ardhi asili yake ni uhaba wa rasilimani ardhi, watu
wanaongezeka ardhi haiongezeki hivyo kutokana na hali hiyo watu
walinyang'anyana ardhi kwa kuingiliana kishuhuli na kusababisha
madhara kama hayo ya mauaji"alisema

Kwa upande wake Emmanuel Papian (mgombea) akijinadi kwa wanachama hao
alisema mgogoro wa ardhi Kiteto asili yake ni ubaguzi,ukabila,pamoja
na rushwa akisisitiza kuwa wananchi wanatambua kiini cha mgogoro tena
kwa kuwataja wahusika kwenye tume zilizoundwa na Waziri Mkuu hivi
karibuni

Alisema akichaguliwa kuwa mbunge wa Kiteto atatawala wananchi wote
bila ubaguzi akidai ripori ya tume iliyoongozwa na Askofu Amos
Mhagachi wa kanisa la MENONITE ataenda kuifufuta kutaka ifanyiwe kazi
ili wananchi wa Kiteto wabaki salama

"Tatizo la mauaji ya Kiteto linasababishwa na baadhi ya viongozi
kuchochea kundi moja la kifugaji kujiona kuwa wao wana haki zaidi ya
wengine na kujichukulia sheria mikononi kuwapiga wakulima, hata mimi
ni mfugaji mbona sijawahi kupelekwa polisi kwa kumpiga
mkulima?viongozi tuacheni tabia ya kuongoza kwa misingi ya ukabila

Kuhusu kauli za uhaba wa rasilimali kiteto Papiani alisema wilaya ya
Kiteto ina km za mraba 16,185,eneo la kilimo ni km za mraba 3800,msitu
wa asili ni km za mraba 1,674 na matumizi mengineyo ni km za mraba 100
uhaba wa ardhi unatoka wapi kama sio ubaguzi alisisitiza Papian

Kwa upande wake Hajjat Amina Saidi Mrisho (mgombea) katika mikutano
hiyo alikanusha vikali kutumwa na wapinzani kugombea Ubunge akisema
anashukuru kwa kumuwamini,akisisitiza kilichomfanya agombee kwa mara
ya nne ni kuhusu mauaji ya mara kwa mara yanayozidi kujitokeza

Kwa upande wake Joseph Mwaleba na Allly Juma Lugendo (wagombea)
walisema waanauwezo mkubwa kama wataalamu wa kuikombea Wilaya ya
Kiteto ambayo kwa sasa inakabiliwa na matatizo mbalimbali yakiwe
uchumi mdogo wa wananchi kutokana na migogoro hiyo

Maoni