SAKATA LA UCHAGUZI KITETO.
Katibu CCM Kiteto afungiwa ndani ya
Ofisi.
·
Wamasai
walinda mlango kwa silaha za jadi
·
Aokolewa
na Polisi,10 wakamatwa
NA.MOHAMED
HAMAD MANYARA.
KATIBU wa
chama cha mapinduzi CCM Wilayani Kiteto mkoani Manyara Abeid Maila, amejikuta
katika wakati mgumu baada ya vijana wa jamii ya kifugaji (morani) masai, kuvamia
ofisi ya chama na kufunga mlango huku wakilinda kwa silaha za jadi.
Tukio hilo
limetokea julay 31 mwaka 2015 saa 4:30 asubuhi baada ya katibu huyo wa CCM
Wilaya kukataa kupokea majina ya wanachama zaidi ya 8000 kata ya Namelock na Sunya yalidaiwa kucheleweshwa
Kwa mujibu
wa taarifa kutoka kwa katibu huyo zilisema, mwisho wa kuwasilisha majina ya
wanachama kwaajili ya maandalizi ya uchaguzi ulikuwa tarehe 15.7.2015 ambapo vijana
hao waliyaleta tarehe 31.7.2015 siku moja kabla ya uchaguzi
“Hatuwezi
kufanya kazi kwa mazoea, hawa vijana niliwaelekeza toka mwanzo kuwa mwisho wa
kuleta majina ya wapiga kura ni julay 15 na hata wagombea wao wanajua
walikwisha kutaarifiwa sasa kitendo cha kulazimisha ni ishara tosha kuwa
wanamsukumo kutoka kwa wagombea wao”alisema Katibu huyo
Alisema
majina ya wanachama wote wa CCM yamewasilishwa mkoani, na idadi inafahamika
hivyo kutenda cha vijana hao kuja na majina hayo ni ishara tosha kuwa wanaanza
kuleta vurugu kutaka kuharibu uchaguzi mzima wa kura za maoni
Wakati
sakata hilo likijitokeza kamati ya Siasa ya Wilaya ilikuwa inaendelea na vikao vyao
kwaajili ya maandalizi ya uchaguzi wa kura za maoni kesho (leo) kwamba
kupokelewa kwa wanachama hao kutampa nafuu mmoja wa wagombea ubunge kati yao
Taarifa za
uhakika kutoka katika vyanzo mbalimbali vya habari hizi zinasema kuwa,
utaratibu huu ndio unaotumika kila mara wilayani humo kujihakikishia ushindi kwa
mgombea ambapo ilielezwa kuwa idadi hiyo ya kura ni nyingi na haijapata kutokea
Kwa Mujibu
wa Joseph Mwaleba mmoja wa wagombea ubunge (CCM) katika maelezo yake na gazeti
hili alisema sakata hili liliibuka siku tatu zilizopita wakimzuia mbunge
anayemaliza muda wake Benedict Ole Nangoro
kulazimisha majina hayo kupokelewa
“Tumekuwa
tukigombana sana na huyu mwezetu kulazimisha vitu nje na sheria, mfano
tuliambiwa mwisho wa kuleta majiana hayo ni tar 15 mwezi huu lakini alizidi
kulazimisha akitaka kiasi hicho kipokelewe jambo ambalo ni kinyume na utaratibu”alisisitiza
Mhombea huyo
Naye Emmanue
Papian Mgombea wa (CCM) na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa alisema mbali
na vioja hivyo, kumekuwepo na ubaguzi wa ukabila uliokuwa unaendelea na kwamba
amezitaka mamlaka husika kuingilia kati na kuona haki ikitendeka kwa maslahi ya
Taifa
“Naviamini vyombo vya usalama vya chama na Taifa
vitatenda haki, kwani kwa miaka zaidi ya 50 sasa hatuwezi kuendelea
kuuzungumzia ukabila na hata ubaguzi wa rangi ni dhambi kubwa na mbaya”alisisitiza
Papian
Kukamatwa
kwa wanachama hao wa CCM na kufikishwa Polisi kumewagawa wajumbea wa
Halamshjauri kuu ya CCM Wilaya kwa msingi wa ukabila ambapo miongoni mwao
walisikika wakisema tutaenda kuwatoa kwa gharama zozote
“Naamini
hilo sio kosa la kutisha, watatoka tu ngoja tumalize kikao hapa, kwani
walichokifanya kiko katika kosa gani la kisheria” alizidi kulalata mjumbe huyo
wa kamati ya Siasa ya CCM Wilaya na kuingia ndani baada ya mlango kufunguliwa
Katibu huyo
wa CCM Wilaya ameripoti polisi kwaajili ya mahojiano zaidi, kwamba mara baada
ya kumaliza anatakiwa kuhakikisha kuwa kesho (leo) uchaguzi unafanyika na
wanachama wa CCM wanapata wawakilishi watatu watakaoenda kuchunjwa mkoani
Kwa upande
wa baadhi ya wananchi walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa hiyo ni ishara
tosha kuwa mwaka huu kutakuwa na mabadiliko makubwa ya utawala, kwani toka
Wilaya izinduliwe mwaka 1974 hayajapata kutokea
Kwa mujibu wa
Jeshi la Polisi Wilaya ya Kiteto zaidi ya vijana 10 wa jamii ya kifugaji wanashikiliwa
kwaajili ya mahojiano zaidi juu ya tukio
hilo na mara baada ya kukamilika
watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zitakazowakabili
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni