Wagombea Ubunge CCM Kiteto waingia
mitini.
·
Wahofu
kuwafanyia fujo,wananchi wawashangaa
NA.MOHAMED
HAMAD KITETO.
MKUTANO wa
kuwanadi makada watano wa chama cha mapinduzi CCM nafasi ya Ubunge kata ya
Kibaya Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, umeingia dosari baada ya wagombea hao
kuingia mitini wakihofia kurushiwa mawe na kuzomewa.
Awali
wagombea hao walifanya mkutano wa kampeni katika kata za Bwagamoyo na Kaloleni
wilayani humo, huku wananchi wakihoji hatma ya maisha yao kuhusu migogoro ya
ardhi kati ya wakulima na wafugaji iliyodumu kwa muda mrefu
Katika
mikutano yote iliyofanyika ya kampeni, wananchi hawakusita kuhoji juu ya
migogoro hiyo, huku wakipatiwa majibu na mbunge anayemaliza muda wake ambapo walidai
kutoridhika wakisema wapatiwa majibu sahihi
“Haiwezekana
hata kidogo kuambiwa eti mbunge wetu hakuhudhuria mazishi na hata kutoa pole
kwa wahanga wa migogoro ya ardhi akidai alikuwa na kazi maalumu…mbona
tunashuhudia maeneo mengine wabunge wao wanakemea vitu kama hivi katika majibo
yao?alihoji mmoja wa wananchi hao
Akizungumza
hayo Bakari Maungaya (mwananchi) alisema kitendo cha wagombea hao kuingia
mitini na kukimbilia vijijini kujinadi inatosha kuwa hawawatendei haki wananchi
hasa wale wanaojitambua mijini na badala yake wanakimbilia vijijini
“Kama kweli
wagombea wanatambua wajibu wao sehemu ya kujipima ilikuwa maeneo ya mijini sasa
kama watawakimbia wananchi wa mijini hawaoni kuwa huko ni kufilisika
kisiasa”alisema huku akionyesha kuchukizwa na tabia hiyo
Hata hivyo
Suleyman Kaberwa mwenyekiti wa CCM kata ya Kibaya akizungumza na umati wa
wanachama hao wa CCM alisema amekerwa na kitendo hicho akisema wengi wa
wagombea hao hawakuwa tayari kufika kwenye eneo hilo la kampeni
“Huko jamani
tumegombana sana kuwakutaka kuja lakini wengi walikataa wakisema wanahofia
maisha yao,baada ya kuona vijana wetu wa bodaboda kupamba msafara wa wagombea
wakati wakitokea kata za jirani”alisema
Kwani
kupambwa kwa msafara kwa mfumo wa kuwa na pikipiki hili ni geni kwenu
jamami?.....hapanaaa sasa tatizo nini hili limeniuma sana najua nimetimiza
wajibu wangu japo kuja kuwaambua kilichotokea alimalizia Kaberwa
Kwa upande
wake Emmanuel Papian akizungumza na Jambo leo kuhusu tuhuma za wagombea kuingia
mitini alisema amekerwa na wenzake ambao mara zote aliwataka waende kwenye
mkutano baada ya kutoka kata za jirani na kukataliwa
“Niliwasihi
sana wenzangu nikawaambia twendeni wananchi wanatusibiri lakiki walionekana kuwa
wazito huku wakisema usalama wao ni mdogo jambo ambalo, niliwaambia kuwa hiyo
ni kazi ya Polisi kutulinda kama kuna shida lakini walikataa
Kwa upande
wa katibu wa CCM Wilaya Abeid Maila alisema ilikuwa vigumu kuwalazimisha
wagombea kuingia kwenye kikao huku wakikataa kwenda hivyo alichofanya ni
kuahirisha kwa kuwataka wajhiandae kumalizia kata ya Kijungu na Loolera
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni