CELG wakabidhi vitendea kazi,wasaidizi
wa kisheria
Na.Mohamed
Hamad Kiteto
KITUO cha
sheria za mazingira na utawala (Center for Enviromental Law and Governance) chenye
makao yake makuu Dar es Salaam, kimetoa msaada
wa vifaa vya ofisi kwa wasaidizi wa kisheria 25 wilayani Kiteto, kwaajili ya
kuwawezesha kuweka kumbukumbu
Vifaa hivyo
ni mafaili ya Ofisi,Scanna moja pamoja na machapisho mbalimbali ambayo
yatasaidia katika kazi ya usaidizi wa kisheria wilayani Kiteto juu ya ukiukwaji
wa haki za binadamu unaoendelea kujitokeza wilayani humo
Akikabidhi
vifaa hivyo kwa mratibu wa wasaidizi wa kisheria wilayani Kiteto mwanasheria wa
kituo hicho Elizabeth Maganga alisema
vifaa hivyo vitumike kuhifadhia taarifa za kituo hicho zinazokusanywa kutoka
kwa wateja wao
“Naamini
sasa taarifa zenu zitakuwa na usiri wa hali ya juu kwani mtakuwa mmezihifadhi
kwenye mafaili, na pia mtatuma taarifa kwetu kwa urahisi kupitia mitandao
ambapo mtaziskan na kuzituma kiurahisi ”alisema mwanasheria huyo
Awali
taarifa hizo zilionekana kutokuwa na usiri wa kutosha pamoja na changamoto za
kutuma taarifa hizo makao makuu jambo ambalo lilikuwa na changamoto kubwa kwa
wasaidizi hao wa kisheria Wilayani humo katika utendaji wao wa kazi
Akishukuru
baada ya kukabidhiwa msaada huo Mwadawa Ally mratibu wa wasaidizi wa kisheria
Wilayani Kiteto alishukuru kituo hicho cha CELG akisema, msaada huo umefika
wakati mwafaka ambao kila mmoja atawajibika katika nafasi yake ipasavyo
“Tulihitaji
kufanya kazi ya usaidizi wa kisheria kwa kiwango cha hali ya juu, sambamba na
kuhifadhi vizuri kumbukumbu zetu sambamba na kuzituma kwa wakati, naamini kazi
hiyo itafanyika kwa umakini wa hali ya juu”alisema Mwadawa
Mbali na
msaada huo washiriki hao wanaendelea na mafunzo ya siku tano kuhusu aina za
ukatili wa kijinsi na sheria zake pamoja na kuunda mikakati ya kuzuia ukatili
wa kijinsia unaoendelea kujitokeza kila kukicha wilayani humo
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni