Mauaji ya Albino nchini bado tishio

Mauaji ya Albino nchini bado tishio

NA.MOHAMED HAMAD DAR
Hofu ya maisha ya watu wenye ulemavu wa ngozi hapa nchini inazidi kutawala kutokana na imani za kishirikina, ambazo zinazidi kujitokeza kwa baadhi ya wanajamii hali inayosababisha wapate ulinzi wa ziada

Hayo yameelezwa na baadhi ya waangalizi wa haki za binadamu waliokutana Jijini Dar kujadili mbinu bora za utoaji wa taarifa za ukiukwaji wa haki za Binadamu kwa njia rahisi wakisema hali si shwari kutokana na viashiria vilivyopo

Akiibua hoja  kwa washiriki hao juu ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na nafasi ya waganga kuhusishwa na mauaji Mkuta Masoli mwanasheria wa LHRC alisema bado tatizo la mauaji linaendelea  huku Serikali ikiwa kimya

Antony Mayunga mwangalizi wa haki za binadamu na mwandishi mkongwe wa gazeti la Mwananchi nchini alisema kila sekta inamapungufu makubwa katika kuhudumia jamii ya watu wenye ulemavu wa ngozi na kuziomba ziondoe mapungufu hayo

"Ukienda kwenye huduma za jamii haziakisi kuwasaidia walemavi hao,nafasi za masomo na kadhalika kuna mapungufu makubwa hii inatokana na kukosekana kwa dhamira ya dhati kwa Serikali katika kukabiliana na tatizo hilo"alisema Mayunga

Naye mmoja wa waangalizi wa haki za binadamu ambaye hakutaka kutajwa majina yake alisema Mpwapwa kuna shule ya watu wenye ulemavu wa ngozi na wasio ona, tatizo lilolopo hapo hawapati mafuta kwaajili ya kulainisha ngozi na kusababisha wapate adha kubwa

Pia alisema pamoja na kuwepo kwa jitihada hizo hawapati fursa mbalimbali za kijamii kama vile uongozi hali inayosababisha wawe na vikundi mbalimbali vya kujitetea katika kukabiliana na tatizo hilo

Kuhusu Suala la elimu kwa jamii kutoka sekta mbalimbali mwangalizi kutoka Mbeya alisema alishuhudia mchungaji mmoja aliita mkutano wa Injili  na kuweka mabango kuwa  dawa ya utajiri ipo pasipo kuua albino

"Walijitokeza watu wengi sana siku hiyo lakini baada ya kuambiwa kuwa wampokee mungu waachane na mauaji ya albino walianza kupungua siku hadi siku kuachana na mkutano huo ambao walihisi kuwa wangeweza kubata utajiri kama walivyotarajia"alisema mwangalizi huyo

Mafunzo  yameandaliwa na Kituo cha Sheria na haki za Binadamu nchini (LHRC) ndani ya mradi wao wa (UHAKIKI ) Ufuatiliaji wa haki za Kisiasa na Kiraia ambayo yamelenga kuunda mpango madhubuti Tanzania bara na Visiwani

Kwa mujibu wa Bernad Sefu msimamizi wa mradi wa UHAKIKI alisema mpango huo utakuwa na manufaa makubwa kwa jamii kwani watapata taarifa sahihi na kwa wakati na kwa njia ya kisasa zaidi ambazo zitasaidia kuanzisha mijadala ya Kitaifa kukabiliana na matatizo ya Nchi

 Mwisho

Maoni