Mbunge viti maalumu CHADEMA Paulina Gekuli akiongea na wajumbe wa BAWACHA Kiteto hivi karibuni, kulia mwenye koti jeusi ni mwenyekiti wa wilaya ya Kiteto CHADEMA tabrani Msangi aliyesimamishwa nafasi hiyo kwa madai ya kumnadi mgombea wa CUF kuwa Mbunge Jimbo la Kiteto
CHADEMA Kiteto wampiga “stop”mwenyekiti
kushiriki kampeni
NA. Mohamed Hamad
Manyara
CHAMA cha
demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoani Manyara, kimemsimamisha kazi mwenyekiti
wa wilaya ya Kiteto Tabrani Msangi, kushiriki kampeni za uchaguzi zinazoendelea
kutokana na madai kuwa amekisaliti chama na kumnadi mgombea wa CUF kwa nafasi
ya Ubunge
Hayo
yalielezwa kwenye uzinduzi wa kampeni za chama hicho kata ya Matui siku moja
baada ya mwenyekiti wa huyo wa wilaya Tabran Msangi kumnadi Hassani Losioki mgombea
wa CUF katika mkutano ulioitwa kuwa ni wa uzinduzi wa Ukawa mjini Kibaya
“Kuanzia leo
Tabran Msangi ni marufuku kushiriki kampeni za CHADEMA zinazoendelea sasa kama
mwenyekiti kutokana na kitendo cha kukihujumu chama kwa kumnadi Hassan Losioki
akidai kuwa ni mgombea aliyetokana na Ukawa”alisema katibu wa CHADEMA mkoa wa
Manyara
Alisema
mwenyekiti huyo toka awali alionekana kuwa msaliti, na chama kilikuwa
kinafuatilia nyendo zake na ndio maana katika hali isiyotazamiwa alijitokeza
hadharani kwenye mkutano wa CUF na kumnadi mgombea wao
Katika kikao
alichoshiriki mwenyekiti Tabrani kumnadi mgombea wa CUF alisema CHADEMA imefanya
mabadiliko ya kumteua mgombea mwingine ambaye ni Hassan Losiok kuwa ndiye
atakayepambania jimbo la Kiteto kuwa Mbunge
Alisema
mgombea Ubunge Kidawa Othman wa CHADEMA hana sifa, ana elimu ya darasa la nne
hivyo hawezi kuingia Bungeni kwa elimu hiyo na nafasi anayoiomba ya Ubunge ni kazi
kubwa ambayo kwa sasa haiwezi
Akiomba ridhaa
kwa wananchi Kidawa Othman alisema, anatosha katika nafasi hiyo na kitendo cha
kuaminiwa na chama chake ni ishara tosha kuwa anauwezo wa kuwatumikia wananchi
katika kujiletea maendeleo ya pamoja
“Siwezi kuwa
mzigo Bungeni,tumekuwa tukikosea sana kuchagua watu wenye sura ya
ukabila,uchoyo na ufisadi katika nafasi ya Ubunge ambao wamekuwa tatizo ambalo
limesababishia wananchi madhara yakiwemo ya maafa”alisema
“Tazama
tumekuwa katika mgogoro mkubwa kati ya wakulima na wafugaji, hii ilisababishwa
na viongozi wetu waliolewa madaraka na kujiingiza katika manufaa yaliyoleta
madhara yakiwemo yale ya watu zaidi ya 40 kuuawa na wengine kujeruhiwa”
Alisema kuwa
atakapochaguliwa kuwa mbunge atahakikisha kuwa anaondoa ukabila uliochimbiwa
mizizi kwa watu kuchukiana kati ya wakulima na wafugaji ambapo ilisababisha
serikali kutumia fedha nyingi kuja Kiteto kufanya uchunguzi juu ya mauaji hayo
mwisho
Maoni
Chapisha Maoni