Dunni akacha mkutano Kiteto
Mohamed Hamad
Kiteto.Mgombea mwenza wa
Urais kupitia vyama vinne vilivyoungana kupitia katiba ya wananchi Ukawa Dunni
Hajji Dunni, ameukacha mkutano ulioandaliwa na CUF wilayani Kiteto kutokana
na mvutano wa kisiasa kati ya CHADEMA na
CUF
Mvutano huo ulimsababisha
Mgombea Urais kupitia Ukawa Endward Lowassa kushindwa kumnadi mgombea wa Jimbo
la Kiteto kutokana na sakata hilo
hivi karibuni ambao kwa sasa siasa za Kiteto zimedaiwa kuchukuwa sura mpya kwa
wananchi
Akiwa mjini Kibaya akitokea
wilaya ya Chemba Dunni aliandaliwa mkutano chini ya viongozi wa CUF wilaya
ambapo walitangazia kuwa watapata fursa ya kumsikiliza mgombea huyo sambamba na
kumnadi mgombea wao wa Ubunge wa Jimbo hilo
kupitia CUF
“Taarifa zilisema kuwa Dunni hajji
atazungumza na wananchi saa 3-4 asubuhi, tulishuhudia wananchi wakiendelea
kusogea kwenye mkutano na baadaye Dunni alitokea katika maeneo ya mkutano bila
kushuka na kuaga baadhi ya viongozi akiwemo Kidawa wa CHADEMA ”alisema mmoja wa
viongozi wa wilaya hiyo
Ujue huu mkutano haukuwa
kwenye ratiba tulishangaa wenzetu wa CUF wakiuandaa kwa nguvu zote na ndio
waliowatangazia wananchi kuwa utafanyika, sasa wananchi wameonekana kuchukizwa sana na kitendo hicho
wakati wakiondoka kwenye mkutano huo,alisema Tikima Rashidi mwenyekiti wa CUF
wilaya ya Kiteto
“Tulitegemea Dunni amtangaze
Hassani Losioki kupitia CUF mgombea ubunge Jimbo la Kiteto ndio anayeungwa
mkono na wananchi, kitendo cha kuondoka ikizingatiwa Lowassa alifika na kuahidi
kuwa hatma ya Kiteto itatokana na maamuzi ya chama makao makuu kuondoka kwake
ametuacha njia panda”alisema Tikima
Mgogoro wa kisiasa kwa
wagombea ubunge wa Jimbo la Kiteto kati ya CHADEMA na CUF unazidi kuchukua sura
mpya baada ya wagombea hao kuzidi kutunishiana mizuli majukwaani kwa
kutuhumiana kuwa ni pandikizi la CCM
Kidawa Othmani anayegombea
kupitia CHADEMA katika mikutano yake alisema kuwa yeye ndiye aliyeteuliwa na
vyama vilivyoungana Ukawa kugombea Jimbo la Kiteto, huku Hassani Losiok naye
katika mikutano yake akiwaambia wananchi kuwa ndiye mgombea pekee
Wakati hayo yakijitokeza
wanachama wa vyama vya upinzani wilayani humo wamedaiwa kuwa njia panda kuona
wagombea hao wakiendelea kusuguana huku zikiwa zimebaki siku chache kuingia
kwenye uchaguzi mkuu ambao watatakiwa kufanya maamuzi
Wadadisi wa masuala ya
kisiasa wakizungumza na gazeti hili walisema mgawanyiko huo ni furaha kwa CCM
ambapo watagawana kura na kumfanya ashinde kwa kura nyingi
“Ujue mvutano huu umetokana
na baadhi ya wagombea ubunge walioangushwa kupitia CCM wafuasi wao kuhamia
vyama vya upinzani na kufanya wananchi washindwe kuwa sasa nani anafaa na kwa
sababu gain,ikumbukwe hata elimu ya uraia haikutolewa”alisema Bakari Maunganya
mwananchi
Mwisho
AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0758 222 248/0787 055080
Email . masarade1995@gmail.com ,
ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE
Maoni
Chapisha Maoni