Habari magazetini millardiayo

Uchambuzi wa magazeti @CloudsFM umekupita? Kazi yangu kila siku asubuhi ni kuhakikisha zile zote kubwa kwenye kuperuzi na kudadis hazikupiti. Kama uliikosa na hukuisikia unaweza kucheki na hizi nyingine kufidia.
Wazungu wa UKAWA wakwama Tanzania, Dk. John Magufuli ang’ara Urais kwenye siku yake ya kuzaliwa, Maalim Seif atoa siku tatu Zanzibar, Edward Lowassa apinga ushindi wa Dk. John Magufuli, Magufuli kupewa cheti chake cha ushindi leo.
Wakati NEC ikimtangaza Dk. John Magufuli kuwa mshindi wa nafasi ya Urais wa Serikali awamu ya tano, Tume hiyo imepiga marufuku kwa vyama vingine kujitangazia matokeo yao ya Urais kwani wenye mamlaka hayo ni wao tu na kwa yoyote atakayejichukulia mamlaka hayo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Waangalizi wa Kimataifa wa Uchaguzi Mkuu 2015, Zanzibar wameitaka ZEC kutaja sehemu ambazo zilikuwa na kasoro kwenye Uchaguzi Mkuu na kuwataka kuweka tofauti zao pembeni na kuendelea na mchakato wa Uchaguzi… Wasomi nchini wametoa mtazamo wao kuhusu Mawaziri na Wabunge walioanguka kwenye Uchaguzi Mkuu na kusema kuwa wananchi wanataka mabadiliko ya utendaji na ndio maana wameamua kuwachagua watu wapya ili kutoa nafasi mpya ya mabadiliko kwenye utendaji kazi.
Baada ya kutokea mzozo kutangazwa kwa matokeo ya Ubunge wa Jimbo la Mbagala hatimaye Mkurugenzi wa Uchaguzi Manispaa ya Temeke amemtangaza mgombea wa CCM, Issa Mangungu kuwa mshindi wa jimbo hilo baada ya kuibuka na kura nyingi zaidi dhidi ya mpinzani wake.
Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania, umewaomba Watanzania kuendelea kuwa watulivu katika kipindi hiki na NEC imefanya kazi nzuri kuhakikisha amani inakuwepo kwa kuzingatia haki, pia imeiomba ZEC kuangalia tena uamuzi waliotoa kuhusu kubatilisha matokeo ya Uchaguzi Mkuu Zanzibar kwa kuwa waangalizi wa Kimataifa walijiridhisha kuwa Uchaguzi huo ulikuwa na ubora wa hali ya juu.
Unaweza kusikiliza uchambuzi wote wa magazeti kwenye #PowerBreakfast hapa chini.

Maoni