Habari wakuu,
Leo aliekuwa mwenyekiti chama cha wananchi (CUF) alifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha Azam TV na mjadala wao ulitawaliwa na kufutwa uchaguzi mkuu Zanzibar na kutoka maamuzi ya kurudiwa. Ameongea kwa kirefu sana lakini kufupisha tu...
Lipumba amesema sababu zilizotolewa na tume ikiwemo waliojiandikisha kuwa wengi zaidi ni mambo ambayo yangeweza kujulikana mapema, pia ameongelea NEC kutangaza matokeo ya Urais yaliyotoka Zanzibar ilihali yamefanyika kwenye uchaguzi huohuo mmoja na tume haijasema uchaguzi ule ulikuwa ni mbovu.
Zaidi ya hapo hata watazamaji wa kimataifa wamesema walau kwenye utaratibu wa kupiga kura na wa kuhesabu kura pale vituoni, utaratibu ule ulikwenda vizuri na CCM kupitia msemaji wao, January Makamba amefanya tathmini na akasema uchaguzi huo kwa ujumla wake umeenda vizuri na akasema watu wasije wakatoa sababu zozote zile za kukataa matokeo.
Inachosikitisha mwenyekiti wa tume amekuja kutangaza kuufuta uchaguzi na ameufuta uchaguzi bila kuwepo kikao rasmi cha tume yoyote ya uchaguzi kujadili suala hilo, hayo ni maamuzi yake peke yake na kufatana na sheria za Zanzibar hana mamlaka hayo, lazima tume ijadili ifikie muafaka na ndipo iweze kutoa maamuzi, ametuletea matatizo kwa sababu hii ni jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Hauwezi kuufuta uchaguzi wa Zanzibar, uchaguzi wa urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ukabaki kuwa sawaswa kwa hio uchaguzi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania hautakua na uhalali ikiwa kura za Zanzibar hazitahesabiwa.
Kwa zaidi aliyoongelea Lipumba yapo kwenye video nilioambatanisha hapa chini.
CHANZO NI JAMIIFORUMS
Maoni
Chapisha Maoni