Malaigwanani Kiteto waridhia
mpango wa uzazi
Na. Mohamed Hamad
Zaidi ya viongozi wa mila mia
moja wa jamii ya kifugaji maasai pamoja baadhi ya viongozi wa Serikali za vijiji
wilayani Kiteto mkoani Manyara, wameazimia kujiunga
na mpango uzazi salama
Wakizungumza kwenye kongamano
lililoandaliwa na Halmashauri ya wilaya kwa ushirikiano na Engenda Helth
viongozi hao wa mila walisema ongezeko la vifo vya wazazi,watoto wachanga na
watoto chini ya miaka mitano linazidi kuwa tishio
“Hatuwezi kuendelea
kushuhudia vifo vya mama na mtoto na kila mara kwa kuendeleza mila na tamaduni
za makabila yetu,kwani madhara tunayaona kazi tutakuwa nayo sasa ni kuhakikisha
elimu hii inawafikia wananchi wetu”alisema Mbambire Oleikurukuru
Alisema kongamano hilo ni matokeo ya kikao
maalumu kilicho fanyika kuwataka viongozi hao ambao wanaushawishi mkubwa ndani
ya jamii kuhamasisha jamii kutumia mpango wa uzazi salama na kuzuia maambukizi
ya VVU Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa motto
Pia mafunzo hayo yalihitaji
wanaume kushiriki huduma za afya ya uzazi,huduma za uzazi wa mpango na uchaguzi
wa saratani ya shingo ya kizazi na mama kuwa salama anapojiandaa kubeba ujauzito
hadi arobaini ya uzazi
Wakati wa ujauzito mama
anatakiwa kuwahi kliniki kabla ya wiki 12 ili aweze kupata huduma zote kama
vile upimaji wa VVU Ukimwi na magonjwa kama vile kaswende,kupima kiasi cha
damu,kupewa dawa za kinga ya malaria na za madini chuma na dawa ya minyoo
Mbali na huduma hiyo pia wazawazito
watapewa ushauri wa masuala ya lishe maandalizi ya kujifungua sambamba na
ugunduzi wa dalili za hatari wakati wa ujauzito,kujifungua na baada ya mtoto
kuzaliwa
Katika kuhakikisha mpango
unafanikiwa wajawazito wametakiwa kujifunguliwa vituo vya huduma kama vile Zahanati,kituo cha afya ama Hospitalini ikiwa
lengo la Kitaifa linatakiwa 80%
Akiwasikilisha takwimu za
hali ya wajawazito kujifungulia vituoni Hadija …Mratibu wa …alisema mwaka 2012
waliojifungulia vituoni ni 2112 kati ya 9180 sawa na 23% huku mwaka 2013
waliojifungulia vituoni ni 2779 kati ya 9786 sawa na 28% huku 2014 walikuwa
3389 kati ya 10423 sawa na 32%
Kuhusu uzuiaji wa maambukizi
ya VVU Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa motto alisema uwezekano endapo mama
hatatumia huduma yoyote ni 5-10% wakati wa ujauzito,10-20% wakati wa uchungu na
kujifungua na 5-15% wakati wa kijifungua
Alisema kuwa lengo la Wizara
ni kupunguza maambukizi hadi kufikia chini ya 5% akisema kwa Kiteto kati ya watoto
73 waliokuwa wamezaliwa 4 sawa na 5% walikuwa na VVU Ukimwi mwaka 2012,2013
kati ya 103 waliozaliwa 7 walikutwa na VVU Ukimwi huhu mwaka 2014 3 kati ya 91
waliokuwa wamezaliwa walikutwa na VVU
Katika kukabiliana na tatizo
hili uongozi wa wilaya kupitia idara ya afya imeendelea kutoa elimu katika
maeneo mbalimbali yakiwemo kwenye vituo vya afya sambamba na mafunzo kwa
walengwa kupunguza VVU Ukimwi
Katika hatua hiyo wameweza
kuwafikia watu maarufu kama vile viongozi wa mila zaidi ya 100 ambayo wanasauti
ndani ya jamii kuwapa elimu ili waweze kuelimisha jamii zao waweze kuondokana
na tatizo hilo
Wakiwa katika mkutano wa
pamoja uliofanyika hivi karibuni kata ya Partimbo baada ya kupata elimu hiyo
viongozi hao kwa pamoja waliadhimia kuunga jitihada za idara ya afya Kiteto za
kupunguza vifo pamoja na maambukizi ya VVU Ukimwi
Walisema kwa kuwa wanaaminika
ndani ya jamii wataenda kuelimisha jamii zao ili waweze kukubaliana na
mapendekezo ya wataalamu ambao wamewataka kuhudhuria kliniki sambana na wenzi
wao
“Elimu hii ni muhimu sana hakuna anayetaka mke
wake ama motto apoteze maisha kwa kutofika kliniki, huko tutakwenda na
tutahamasisha wenezu waweze kuona umuhimu wa kufika kwa wataalamu”alisema
Lemomo Moringe (laigwanani)
Alisema jamii ya kifugaji
inachangamoto kubwa ikiwemo kuwa na wake wengi wakidai suala la kuhudhuria kila
mara kiliniki litawapa ukumu kulingana na kazi zao na kuomba Serikali ijenge
vituo vya afya karibu nao ili wae na uwezo wa kufika sambamba na upatikanahi wa
huduma bora yakiwemo madawa
“Unaweza kwenda Zahanati ya
Serikali ukaambiwa kanunua dawa kwenye maduka ya watu binafsi hili
linatukatisha tamaa sana
na wakati mwingine tunashawishika wake zetu kujifungulia kwa wakunga wa
jadi”alise,ma Lemomo
Kwa mujibu wa taarifa toka
Serikalini zinaeleza kuwa mpango uliopo kila kijiji kinatakiwa kujenga Zahanati
huku kata ikitakiwa kujenga kituo cha afya na Wilaya kuwa na Hospitali ya
wilaya ili kupunguza adhaa na usumbufu wa upatikanani wa huduma ya afya
Mwisho
AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0758 222 248/0787 055080
Email . masarade1995@gmail.com ,
ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE
Maoni
Chapisha Maoni