Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Mbatia: Hauwezi ukafuta uchaguzi wa Zanzibar ukaacha uchaguzi wa Jamhuri ya muungano

Habari wakuu,

Mchana wa Leo baada ya tume ya uchaguzi Zanzibar(ZEC) kufuta matokeo kwa upande wa Zanzibar, mwenyekiti wa chama cha NCCR na mwenyekiti mwenza kwenye umoja wa katiba ya wananchi(UKAWA) aliongea na wanahabari na yafuatayo ni mazungumzo yake.

MBATIA: Lowassa ni mgombea Urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania sio mgombea Urais wa Tanganyika, wanaosimamia uchaguzi kwa upande wa Zanzibar kwa lugha nyingine ni mawakala wa NEC, kwa upande wa Zanzibar ni ZEC, tume ya uchaguzi wa Zanzibar(ZEC) bila kushauriana na alieshinda, Maalim Seif Shariff Hamad, bila mwenyekiti wa ZECkushauriana na makamishna wenzake, kwa shinikizo la serikali ya Jakaya Mrisho Kikwete, kwa shinikizo la chama cha mapinduzi na kwa kuwa Maalim Seif alikuwa ameshinda uchaguzi wa Rais wa Zanzibar, mwenyekiti wa ZEC ametamka kuwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar umefutwa, ndicho kinachoendelea Zanzibar sasa.

Wamesema ni kutokana na irregularities, nimeongea na Maalim Seif sasa hivi, nimeongea na mheshimiwa Duni sasa hivi, nimeongea na authorities zinazohusika ni kwamba wamefuta uchaguzi mkuu Zanzibar kwa sababu Maalim ameshinda, hauwezi ukafuta uchaguzi wa Zanzibar ukaacha uchaguzi wa Jamhuri ya muungano, upande mmoja wa jamhuri ya muungano umeshafuta uchaguzi na wametamka wamefuta uchaguzi mkuu, kama umeshafuta uchaguzi mkuu wa upande mmoja wa jamhuri ya muungano, upande mmoja unasubiri nini?

Kwa hivyo huu ni mgogoro mkubwa, Damian Lubuva tunachomtaka, anachoendelea nacho sasa hivi ni kiini macho, anajifurahisha tu mwenyewe na ni kinyume cha katiba, Lubuva huku anatamka, mwenzake kule anafuta. Tupo kwenye mgogoro mkubwa wa kikatiba, lililotokea mwaka huu upande wa Zanzibar ni kwamba uchaguzi mkuu automatically haupo, inabidi sasa kukaa na kufanya utaratibu upya wa uchaguzi, kama ukiwa kule umefutwa na huu utakuwa umefutwa na kwa kuwa tunaenda kwenye vikao vyetu basi tutajadiliana alafu baadae tutawabrief.

Chanzo jamiiForums

Maoni