MBUNGE WA LUDEWA AFARIKI KWA AJILI YA HELKOPTA

MBUNGE WA LUDEWA AFARIKI KWA AJILI YA HELKOPTA



Mwili wa Deo Filikunjombe ukitolewa Eneo la tukio baada ya kuteketea kwa Moto kufuatia ajali ya helkopta iliyotokea jana Jioni .

Shuhuda wa ajali hiyo ambaye anamiliki kitalu cha uwindaji na kwamba game guide wao ndiye aliyeona ajali ikitokea na kuwaka moto mkubwa majira ya saa 11 na nusu jioni wakati ikitaka kutua ktk airstrip yao Msegule Airstrip   Na baadae kuitaarifu TAA.

Waliofariki mbali ya Filikunjombe wengine ni Mwenyekiti wa TLP Mkoa wa Iringa Blanka Francis Haule ,Egdi Francis Nkwela na rubani wa helkopta hiyo Wiliam  Slaa.

Miili yote imepelekwa jijini Dar esalaa kutoka katikati ya mbuga ya Selou kitalu R3 ,mwili wa Filikunjombe utaagwa kesho jumamosi jijini  Dar na kusafirishwa kwenda Ludewa kwa mazishi yatakayofanyika jumapili .
 
 
WASILIANA NAMI KWA 0787 055080 / 0758 222248

Maoni