MREMA AMWOMBEA KURA MAGUFULI JAPO CHAMA CHAKE KIMESIMAMISHA MGOMBEA

Hii ni moja ya sura ya hali halisi ya siasa za uchaguzi wa viongozi inavyoendelea nchini Tanzania kwa wakati huu, ambapo Mwenyekiti wa TLP, Augustino Mrema ambaye anatetea kiti chake cha Ubunge kwa jimbo la Vunjo, leo alijotokeza kwenye msafara wa mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM), John Magufuli na kudai kuwa anamuunga mkono, licha ya chama chake, TLP kuwa na mgombea katika nafasi hiyo, Macmillan Lyimo.

Mrema amewataka wananchi wa jimbo la Vunjo kumpa kura za Urais Magufuli lakini kura zote za ubunge wampatie yeye.

Mrema anakabiliwa na upinzani mkali jimboni Vunjo kwani atapambana na Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia ambaye anawakilisha umoja wa vyama vinavyounda UKAWA (NCCR, CHADEMA, CUF na NLD) na hivyo kumuweka kwenye wakati mgumu wa kutetea ubunge wake.

CHANZO MATUKIO DAIMA

Maoni