Na. Mohamed Hamad
MWENGE wa Uhuru Wilayani Kiteto mkoani Manyara umezindua, umekagua na
kuweka mawe ya msingi miradi ya thamani ya bil 2,160,949,120, kama
moja ya kichocheo cha maendeleo ya wananchi
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Kanal Samuel Nzoka akikabidhiwa Mwenge huo
katika Kijiji cha Ndedo Wilayani Kiteto ukitokea Simanjiro jana
alisema Mwenge wa Uhuru utatembezwa umbali wa km 362 wilayani humo
Alisema Mwenge utazindua miradi nane ukiwemo Jengo la Benki mazao
kikundi cha Upendo vikoba Ndaleta lililojengwa kwa thamani ya Tsh
23,000,000 kwa ushirikiano wa Halamshauri, Wahisani pamoja na jamii
Kwa mujibu wa Risala iliyosomwa mbele ya kiongozi wa mbio za Mwenge
Juma Khatib Chumu alielezwa kuwa S Shirika la msalaba mwekundu
limechangia mil 21 na Halmashauri mil 1 ukilenga kutoa msaada wa
chakula kwa wananchi wenye mahitaji
“Makundi maalumu kama vile wazee,yatima,walemavu na wajane yananufaika
sana na huduma hii kwani wamekuwa wakipata msaada unaotokana na kazi
zinazofanyika kama moja ya lengo kuu”ilisema risala hiyo
Mradi mwingine ni jengo la kituo cha wakulima Njoro lililowekwa jiwe
la msingi lenye thamani ya mil 83 ambapo wahisani walichangia mil 68,
jamii mil 13 na Halmashauri ya wilaya ya Kiteto mil 2
Barabara ya km 32 kutoka Kijiji cha Kiperesa hadi Matui ya thamani ya
bil 1,294,148,500 ilifunguliwa na mwenge ambapo wahisani walichangia
bil 1,292,148,500 na Halmashauri ilichangia mil 2
Miradi mingine uliowekwa jiwe la msingi ni kisima cha maji Kijiji cha
Chapakazi matui wenye thamani ya mil 606,629,391, wahisani mil
602,629,391 Halm mil 4 ambapo utakuwa na manufaa kwa watu na mifugo
Mradi mwingine uliofunguliwa na Mwenge ni Jengo la mama na mtoto kituo
cha afya Engusero lenye thamani ya mil 60,682,979 ambapo kiongozi wa
Mbio za mwenye alitoa chanjo kwa watoto wawili kituoni hapo
Mwenge wa Uhuru ukiwa mjini Kibaya ulikagua kikundi cha ujasiria mali
cha wanawake UPENDO ambacho kwa mujibu wa taarifa yao wanajukumu la
kutoa misaada mbalimbali ndani ya jamii
Pia ulifungua AWABOMA SACCOS Kibaya pamoja na kufungua mradi wa
ufyetuaji wa tofali kwa kutumia mashine ya Hydroform wa thamani ya mil
1,605,000 ambapo kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa anye alifatua
tofali kama majaribio
Akizungumza na wananchi katika maeneo mbalimbali wilayani Kiteto Juma
Khatibu Chumu kiongozi wa mbio za mwenge aliwapongeza wananchi
kushiriki shuhuli za kiuchumi kikamilifu kwa lengo la kuondokana na
umaskini
Pia aliwataka wananchi wenye sifa za kushiriki uchaguzi kujitokeza kwa
wingi ili waweze kuwachagua viongozi mwaka huu ambao watakuwa na
jukumu la kuwaongoza katika maeneo yao
“Chagueni viongozi mwenye sifa za kuhubiri amani na wapatikane kwa
njia ya amani bila maandamani na sio wenye sifa ya wizi,wenye sera na
mipango ya kulikomboa Taifa na umaskini wa kipato na sio kiongozi
mwenye kujilimbikizia mali”alisema
Alisema Kiteto inatatizo la migogoro ya ardhi kati ya wakulima na
wafugaji na kuwataka watu kuacha kujichukulia sheria mikononi,akisema
Tanzania inasifika kama kisiwa cha amani Duniani
Alitaja baadhi ya Chamangamoto zilizopo nchini kuwa ni pamoja na
Rushwa,madawa ya kulevya ambayo alidai kila mtu anatakiwa kuwa mlinzi
wa mwenzake kuepukana na uhalifu wa namna hiyo
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX
AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0758 222 248/0787 055 080 Email . masarade1995@gmail.com ,
ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE
Maoni
Chapisha Maoni