Mwenyekiti UV-CCM Kiteto mbaroni



Mwenyekiti UV-CCM Kiteto mbaroni

·        Ni kwa kushambulia gari la mgombea wa Ubunge CUF

Na. Mohamed Hamad
Kiteto.Mwenyekiti wa UV-CCM Wilayani Kiteto Emmanuel Keiya anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuchana picha za mgombea Ubunge kwa tiketi ya CUF  na Urais kupitia Ukawa pamoja na kupora bendera zilizokuwepo kwenye gari

Kamanda wa  Polisi mkoani Manyara Kamishna msaidizi Kristopher Fuime amethibitisha kutokea tukio hilo akisema, Jeshi la Polisi Kiteto linaendelea na uchunguzi zaidi na mara utakapokamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zitakazo mkabili

Kamanda Fuime alisema tukio hilo lilitokea Oct 10 mwaka huu saa mbili asubuhi mjini Kibaya wakati Gari namba T 887 DDB la mgombea Ubunge Jimbo la Kiteto Hassani Losioki likiendeshwa na Amiri Iddi Msemo kukutana na vijana wa CCM Greengurd na kusimamishwa kisha kuanza kulishambuliwa

“Kwa sasa Polisi tunafanya uchaguzi wa kina kutaka kujua kiini cha tatizi hilo na kwamba mara baada ya uchunguzi kukamilika tutalifikisha mahakamani kwaajili ya hatua zaidi zkisheria”alisema Kamanda Fuime

Kwa mujibu wa dereva huyo alisema, siku hiyo alikuwa anaenda kumchukua Bosi wake mgombea Ubunge Jimbo la Kiteto kupitia Ukawa Hassani Losioki na ndipo alipokutana na vijana hao njiani na kumtaka ashuke chini kisha kuanza kulishambulia gari lake

Alisema vijana hao walichukua bendera zilizokuwa kwenye gari ikiwemo ya CHADEMA,CUF na NCCR Mageuzi kisha kuchana picha zote zilizokuwa zimebadikwa kwenye gari hilo ikiwemo za mgombea huyo na ya Ukawa

“Walichofanya vijana wa CCM waliokuwa makundi mawili yakiimba nyimbo za chama hicho wakiongozwa na mwenyekiti wao ni kuchana bendera za vyama vilivyoungana Ukawa zilizokuwa zinapepea pamoja na mabango kisha kupiga dari na kusababisha kreki kioo cha mbele”alisema Dereva huyo

Alisema wakati wakiondoka mwenyekiti wao alisema kuwa hiyo ni trela wanataka kuja kuichoma gari hilo, hivyo awe makini kwani hawataki mchezo,alisema dereva huyo huku akishukuru kuwa hakushambuliwa kupigwa dhidi ya uharibifu huo wa gari

Nao baadhi ya wananchi Wilayani Kiteto akiwemo Maulidi Kijongo,Bakari Maunganya pamoja na Haalima Ndaira walisema kywa kwa siku mbili mfululizo waliona vijana hao nyakati za usiku saa kumi na moja asubuhi wakiimba nyimbo za chama mitaani

Walisema kitendo hicho kiliwatishia sana huku wakijua kuna vyombo vya sheria ambavyo vilitakiwa kuzuia mara moja lakini vilibaki kimya mpaka yakajitokeza ambayo kwa sasa sheria inatakiwa kchukuwa mkondo wake

Kwa Upande wake Boscko Ndunguru Msimamizi wa Uchaguzi wilayani humo kuhusu tukio hili amesema bado  halijawasilishwa ofisini kwake huku akidai kuwa ni la kisheria na sio la kisiasa

“Sheria itafuata mkondo wake,sheria za uchaguzi ziko wazi kila mtu akitaka kujua ni rahisi tuu ukifanya kosa umedhamiria, kwahiyo sheria itafuata mkondo wake mimi sina la zaidi”alisema Ndunguru
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0758 222 248/0787 055080
Email . masarade1995@gmail.com ,
ANGALIZO KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE

Maoni