NEC,VYAMA VYA SIASA VYAZIDI KUVUTANA KUHUSU HATMA YA WAPIGA KURA
Upo mgongano wa maslahi
kati ya Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) na vyama vya siasa juu ya
mustakabali wa wapiga kura hapo Oktoba 25.
Utata huo unatokana na utekelezaji wa Sheria ya Uchaguzi inayoagiza wananchi kutokuwepo vituoni baada ya kupiga kura.
Kifungu
cha 104 (1) cha Sheria ya Uchaguzi, Sura ya 343 inasema, mtu yeyote
haruhusiwi kufanya mkutano siku ya uchaguzi au ndani ya majengo ambako
upigaji kura unaendelea au sehemu yoyote ndani ya mita 200 ya jengo hilo
akiwa amevaa au kuonyesha bango, picha au nembo kwa ajili ya kumpigia
debe mgombea kwenye uchaguzi huo.
NEC
wameagiza watu wasiwepo kabisa hata kwa umbali huo unaosemwa na sheria
na badala yake waende nyumbani ilhali vyama vya siasa vinawataka wafuasi
wao wawepo kwa lengo la kusubiri matokeo. Jeshi la Polisi nalo limesema
halitokuwa na mjadala na mtu asiyetii sheria kwa shuruti.
Pamoja
na mapenzi au mahaba yaliyopo dhidi ya misimamo ya kiitikadi ni vyema
kila mwananchi akawa makini na siku hiyo kwa kutambua anachotakiwa
kufanya ili kuepusha madhara yoyote yanayoweza kuharibu maisha ya
baadaye wakati yule unayempigania akiendelea kusherehekea ushindi
alioupata kupitia juhudi zako.
KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA SIMU NAMBA 0787 055080.0758 222248
Maoni
Chapisha Maoni