Polisi Kiteto wasaka watu wanaotuhumiwa kuchomwa moto Kanisa

 Polisi Kiteto wasaka watu wanaotuhumiwa kuchomwa moto Kanisa

NA.MOHAMED HAMAD
Jeshi la polisi wilayani Kiteto mkoani Manyara, linawasaka watu wasiojulikana kwa tuhuma za kuchoma kanisa la Anglikan, eneo la pandisha kata ya Bwagamoyo wilayani Kiteto

Kuchomwa kwa kanisa hilo kumesababisha zaidi ya waumini 100 kukosa mahali pa kuabudia na kulitaka Jeshi la Polisi, kuwasaka wahalifiu hao na kuwafikisha mahakamani kujibu tuhuma hizo

Baadhi ya wananchi wilayani Kiteto wameonyesha hisia zao mara baada ya kuchomwa kanisa hilo kuwa ni kitendo kiovu ambacho hakipaswi kuigwa

Kwa upande wa Uongozi wa kanisa la Anglikan kuhusu kuchomwa kwa kanisa hilo hapa waliwataka Jeshi la polisi kuwasaka wahalifu hao na kuwafikisha kwenye mikono ya sheria

Katika kuhakikisha kuwa amani inaimarika Jeshi la polisi linawajibu mkubwa wa kulinda raia na mali zao, na bila shaka kwa muungwana yoyote hawezi kufurahishwa na vitendo vya uvunjifu wa amani
Kutoka

xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

 AHSANTE KWA KUENDELEA KUPATA HUDUMA ZETU PIA KUJITANGAZA NASI IWAPO UNAHABARI AMA TANGAZO WASILIANA NASI 0758 222248 Email .masarade1995@gmail.com

ANGALIZO NDG YANGU..
KUMBUKA KILA MMOJA ANA MTAZAMO WAKE HIVYO TUMIA LUGHA NZURI KATIKA KUTOA MAONI YAKO IWAPO UTASHINDWA BASI NI HERI USITOE MAONI SI LAZIMA ILI KUEPUSHA MAKWAZO KWA MWINGINE

Maoni