|
TUME
YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
Kitalu
Na. 8, Mtaa wa Luthuli
S.L.P
2643, DAR ES SALAAM
Simu:
+255 22 2135747/8; 2137125; 2135222
Faksi:
+255 22 2111281
Barua
Pepe: chragg@chragg.go.tz
Tovuti:
www.chragg.go.tz
|
Oktoba 27,
2015
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imepokea kwa masikitiko
makubwa taarifa za vurugu zinazotokea katika maeneo mbalimbali nchini wakati huu
wa kusubiri kutangazwa rasmi kwa matokeo ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na
Madiwani uliofanyika Oktoba 25, 2015.
Aidha, Tume imesikitishwa na hatua ya baadhi ya wanasiasa kuingilia
majukumu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC),
ikiwa ni pamoja na kujitangazia matokeo ya uchaguzi kinyume cha taratibu na
sheria za uchaguzi.
Tume inapenda kuchukua fursa hii kukemea vitendo hivyo vinavyofanywa na
wanasiasa na wafuasi wao ambavyo siyo tu vinaashiria uvunjifu wa sheria,
taratibu na kanuni za uchaguzi ambao unaweza kusababisha uvunjifu wa amani na
utulivu, haki za binadamu na vitendo vinavyokwenda kinyume na misingi ya
utawala bora.
Kwa taarifa tulizonazo vurugu hizo zinazotokea katika maeneo machache ya Tanzania
Bara na Zanzibar zimelilazimu Jeshi la Polisi kutumia nguvu, ili kuhakikisha
kuwa utulivu na amani ambao tumeushuhudia unaendelea.
Kwa kuwa nchi yetu inaongozwa na utawala wa sheria, Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora inawataka wadau wote wa uchaguzi waongozwe na sheria
za nchi.
Kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi, zinazosimamiwa na NEC na ZEC Tume za
Uchaguzi ndizo zenye mamlaka ya kutangaza matokeo ya uchaguzi.
Ili Taifa letu liendelee kuwa
na utulivu katika kipindi hiki cha kusubiria kutangazwa rasmi kwa matokeo ya
uchaguzi Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora:
1.
Inawataka
wadau wote wa uchaguzi wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa, wagombea,
watendaji wa mamlaka za uchaguzi, na Serikali kuheshimu sheria za uchaguzi na kila
mmoja kutimiza wajibu wake.
2.
Tume
(THBUB) inawakumbusha Wagombea wasijitangazie matokeo yao wenyewe ili kuepuka uvunjifu
wa sheria na mkanganyiko unaoweza kusababisha vurugu na uvunjifu wa amani.
3.
Aidha,
THBUB inawataka wanasiasa na wananchi kwa ujumla wawe watulivu na wasiziingilie
kazi za NEC na ZEC.
4.
Inawasihi
wanasiasa, wagombea na wananchi kwa ujumla wawe watulivu katika kipindi hiki
cha kusubiri matokeo rasmi na wajiepushe na vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa
amani na haki za binadamu. Kama kuna malalamiko yoyote, sheria na taratibu
stahiki zifuatwe
Tume inawataka wananchi watakaobaini uvunjifu wowote wa
haki za binadamu, au uvunjifu wa sheria ya uchaguzi, kuzijulisha mamlaka husika
zinazosimamia zoezi la uchaguzi. Aidha, wanaweza kutoa taarifa Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora kupitia ujumbe mfupi wa simu ya kiganjani (SMS) kwenda
Na. 0754 460 259.
Ujumbe lazima uanze na neno 'TAARIFA' au ' RIPOTI' kisha
andika taarifa yenyewe. Namba hii inapokea ujumbe mfupi tu. Kwa taarifa zaidi
piga Na. +255 22 2135747- 8.
Imetolewa na:
(SIGNED)
Bahame Tom Nyanduga
Makamu Mwenyekiti
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
Oktoba 27, 2015
WAANGALIZI WA ULAYA
WATOA MAONI KUHUSU UCCHAGUZI MKUU TANZANIA
Waangalizi wa Umoja wa Ulaya wamesema uchaguzi wa Tanzania kwa kiasi
kikubwa umeendeshwa vizuri lakini kasoro kadhaa zimesababisha baadhi ya
wanasiasa kutilia shaka uhuru wa Tume za Uchaguzi NEC na ZEC.
Katika tamko lao la awali mbele ya waandishi wa habari waangalizi hao
wamesema kuwa uchaguzi wa mara hii ulikuwa na ushindani mkali huku
kukishuhudiwa idadi kubwa ya watu wakijitokeza kupiga kura katika hali
ya utulivu na amani.
Waangalizi hao wamesema kuwa pamoja na kwamba tume hizo zilijiandaa
vyema kufanikisha uchaguzi huo lakini kutokuwepo kwa dhana ya uwazi na
kukosekana kwa maelezo muafaka kuhusu daftari la kudumu la wapiga kura
kumesababisha kujitokeza kwa hisia mbaya kwa vyama vya siasa juu ya tume
hiyo.
Waangalizi hao wamesema kuwa mambo hayo kumesababisha pia kwa vyama vya
siasa kupoteza imani juu ya mchakato huo wa uchaguzi.
Akisoma tamko hilo, Mwangalizi Mkuu wa Umoja huo wa Ulaya, Judith
Sargentini, alisema kuwa alikaribisha namna ushindani mkubwa
uliojitokeza kwenye uchaguzi wa safari hii, lakini akasisitiza kuwa
tamko hilo ni la awali kwa vile bado shughuli za uchaguzi zinaendelea.
“Napenda kusisitiza hili kwamba, taarifa hii inatolewa wakati ambapo
kazi ya kujumlisha matokeo ingali ikiendelea, hivyo ifahamike kwamba
taarifa hii siyo tamko la mwisho kuhusiana na tathmini ya waangalizi wa
Umoja wa Ulaya," alisema Sargentini na kuongeza.
"Tunavyozungumza waangalizi wetu wanaendelea kufuatilia zoezi la
ujumlishaji wa matokeo.”
Umoja wa Ulaya ni sehemu ya waangalizi wa kimataifa walioko nchini kwa
ajili ya kufuatilia uchaguzi huu ambao pia umeshuhudia baadhi ya vigogo
wa kisiasa wakiangushwa kwenye majimbo yao.
Waangalizi wengine ni pamoja na Umoja wa Afrika na wale kutoka Jumuiya
ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC.
Aidha waangalizi hao wa Ulaya wamesema wataendelea kusalia nchini hadi
hapo Novemba 15, katika kipindi hicho itajihusisha na majukumu kadhaa
ikiwamo kukutana na vyama vya siasa, maofisa wa uchaguzi wa asasi za
kiraia.
Umoja huo umetuma jumla ya waangalizi 141 waliosambazwa katika vituo
vyote 625 vya upigaji wa kura. Huu ni ujumbe mkubwa zaidi kuwahi kutumwa
na umoja huo kufuatilia uchaguzi wa Tanzania.
Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu

Maoni
Chapisha Maoni