Ukatili wa watoto Kiteto wakithiri


Mamia ya wananchi wa mji wa kibaya wilayani Kiteto mkoani Manyara, wamelaani kitedo cha mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la DOTO kuwafungia ndani watoto wake wadogo wawili mapacha wa umri wa miaka miwili na kwenda zake kazini

Tukio hilo limedaiwa kujirudia ambapo hii leo imedaiwa kuwa ilikuwa arobaini ya  mwanamke huyo baada ya ummati mkubwa wa wananchi hao kuvamia nyumba hiyo baada ya kusikia watoto hao wakilia

Kwa mujibu wa taarifa za majirani zinaeleza kuwa watoto hao huwa wanafungiwa kuanzia saa 12 za asubuhi hadi mama yao atakapotoka kazini ambapo hii leo alilazimika kuitwa saa tano baada ya kutoka asubuhi

Maoni