Tunawaletea matokeo rasmi kwa nafasi ya Ubunge kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC kama yanavyotangazwa na Wakurugenzi wenye dhamana hiyo
Updates: Majira ya Saa kumi na nusu alfajiri. Waitara Mwita wa CHADEMA
ametangazwa kunyakua kiti cha Ubunge Ukonga, kwa kumbwaga Jerry Slaa wa
CCM ambaye alikuwa mpinzani wake mkubwa.
Jimbo la Bagamoyo: Dk Shukuru Kawambwa (CCM) 26,434, Andrew Kasambala (CUF) 16,330, Mwamini Saidi (UMD) 418 na Saidi Athman (ACT Wazalendo) 418.
Jimbo la Ngara:
Alex Gashaza (CCM) 53,387, Dk Bujari Simon (Chadema) 35,254, Helen Gozi
(NCCR-Mageuzi) 997 na Dotto Jasson Bahemu (ACT Wazalendo) 440.
Jimbo la Msalala: Ezekiel Maige (CCM) 36,010, Paulo Malaika(Chadema) 20, 124, Marco Suwa (ACT Wazalendo) 672 na Abeid Ibeshi (UDP) 251.
Jimbo la Busega: Dk Raphael Chegeni (CCM) 40,977, David William (Chadema) 26,995 na Zangi Robart (UDP) 802.
Jimbo la Mbogwe: Augustino Masele (CCM) 32,921, Nicodemus Maganga (Chadema) 13,975 na Andrew Mnuke (ACT Wazalendo) 5,464.
Jimbo la Bukombe: Dotto Biteko (CCM) 47,147, Profesa Kulikoyela Kahigi (Chadema) 29,929 na Dick Bagamba (ACT Wazalendo) 1,673.
Jimbo la Babati Mjini: Pauline Gekul (Chadema) 21,970 na Kisyeri Chambiri (CCM) 16,434.
Jimbo la Kahama Mjini: Jumanne Kishimba (CCM) 47,553, James Lembeli (Chadema) 30,122 na Bobson Wambura (ACT Wazalendo) 605.
Jimbo la Kibaha Mjini:
Silvestry Koka (CCM) 31,462, Paul Mtally (Chadema) 24,860, Habibu
Mchange (ACT Wazalendo) 3,438, Gombati Waziri (CCK) 259, Betha Mpata
(APPT), 120 na Kibona Ally (AFP) 108.
Jimbo la Geita Mjini: Kanyasu John (CCM) 34, 953, Rogers Ruhega (Chadema) 26, 303 na Malebo Michael (CUF) 625.
Jimbo la Mkinga: Dustan Kitandula (CCM) 21,623, Bakari Kassimu (CUF) 13, 547, Rachel
Sadick (Chadema) 3,789 na Ali Mwita (ACT Wazalendo) 402.
Jimbo la Lindi Mjini:Selemani Kaunje (CCM) 20,733 na Salum Barwany (CUF) 18, 843
Jimbo la Same Mashariki: Naghenjwa Livingstone Kaboyoka wa Chadema, amemshinda Anne Kilango Malecela kwa jumla ya kura 18836, dhidi ya kura 15539.
Updates: Mgombea Ubunge Jimbo la Mwanga Prof. Jumanne Maghembe wa CCM ameibuka kidedea na kutetea kiti chake cha Ubunge
-Amembwaga Henry Kileo wa CHADEMA
Updates: Wilfred Lwakatare (Chadema) kapata kura 28, 112 na kumshinda Balozi Khamis Kagasheki (CCM) aliyepata kura 25, 565
Updates:Jimbo la Vunjo, Kilimanjaro; Mgombea wa NCCR Ndg. James Mbatia,
ameshinda kiti cha Ubunge kwa kuzoa kura 60,187 akifuatiwa kwa mbali na
mgombea wa CCM Innocent Melleck Shirima aliyeambulia kura 16,097.
Updates:Jimbo la Moshi Vijijini, Kilimanjaro; Mgombea wa CHADEMA Anthony Calist
Komu ameshinda kiti cha Ubunge kwa kuzoa jumla ya kura 55,813,
akifuatiwa kwa mbali na mgombea wa CCM Dr. Cyril Chami ambaye pia
alishawahi kuwa Waziri Viwanda na Biashara aliyepata kura 24,415.
Updates:Jimbo la Nyamagana, Mwanza: Mgombea wa CCM, Mabula Stanslaus Shing'oma
ameshinda kwa kuzoa kura 81,017, akifuatiwa kwa karibu na Ezekiel Wenje
wa CHADEMA aliyeambulia kura 79,280.
==>CCM pia imeshinda Kata 14 kati ya 18 za udiwani katika Jimbo la Nyamagana huku Chadema kikiambulia Kata Nne, hivyo CCM itaunda Halmashauri ya Nyamagana.
==>CCM pia imeshinda Kata 14 kati ya 18 za udiwani katika Jimbo la Nyamagana huku Chadema kikiambulia Kata Nne, hivyo CCM itaunda Halmashauri ya Nyamagana.
Updates:Jimbo la Tarime vijijini, mkoani Mara: Mgombea wa CHADEMA, Heche John
Wegesa ameibuka kidedea kwa kupata kura 47,249, huku akifuatiwa kwa
karibu na Kangoye Christopher Ryoba wa CCM aliyepata kura 42325.
Updates:Jimbo la Chato, mkoani Geita: Mgombea wa CCM, Dr. Kalemani Matogolo Medard ameibuka mshindi kwa kupata kura 78,817 akifuatiwa na Lukanima Benedicto Kulwizira wa CHADEMA aliyepata kura 32,513.
Updates:Mgombea wa CCM katika jimbo la Ilala, jijini Dar es salaam, Azzan Mussa Zungu ameibuka kidedea kwa kupata kura 35,818 dhidi ya kura 32,533 za Muslim Haiderali Hassanali wa CHADEMA
Update: Mgombea
ubunge jimbo la Kasulu mjini kupitia chama cha ACT Wazalendo, Moses
Machali amepoteza jimbo hilo, ameshindwa na Mgombea wa CCM Daniel Sanze.
-Amepata kura 22,512 na mshindi Daniel wa CCM amepata kura 25,336
Updates:Matokeo ya ubunge Iringa Mjini kutangazwa kesho baada ya kuchelewa kupatikana kwa matokeo ya kituo cha Kata ya Ruaha.
-Amepata kura 22,512 na mshindi Daniel wa CCM amepata kura 25,336
Updates:Matokeo ya ubunge Iringa Mjini kutangazwa kesho baada ya kuchelewa kupatikana kwa matokeo ya kituo cha Kata ya Ruaha.
Updates:Joram Hongoli wa Chama cha Mapinduzi (CCM) atangazwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Lupembe kwa kupata jumla ya kura 20,430 na kumwangusha mpinzani wake toka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Edwin Swalle aliyepata jumla ya kura 10407
Updates: Jimbo la Mchinga: Hassan Bobali wa CUF, ameshinda kwa jumla ya kura
14776, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Saidi Mtanda wa CCM, aliyepata
kura 13665
Updates:Jimbo la Singida Magharibi: Kingwi Immanuel wa CCM, ameshinda kwa jumla
ya kura 25102, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Allute Mdinka wa
Chadema, aliyepata kura 13480
Updates:Jimbo la Singida Mashariki: Tundu Lissu wa Chadema, ameshinda kwa jumla
ya kura 25010, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Jonathan Njau wa CCM,
aliyepata kura 18614.
Updates: Jimbo la Singida Mjini: Mussa Sima wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura
36690, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Mgana Msindai wa Chadema,
aliyepata kura 16702
Updates:Jimbo la Mtama: Nape Nnauye wa CCM, ameshinda kwa jumla ya kura 28110,
dhidi ya mpinzani wake wa karibu Suleiman Luwongo wa Chadema, aliyepata
kura 13918
Updates: Cecil Mwambe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) apata kiti cha Ubunge katika Jimbo la Ndanda mkoani Mtwara kwa kuwa na kura 26,247, huku Mariam Kasembe wa Chama cha Mapinduzi kukikosa kiti hiko kwa kupata kura 26,215
Updates:Jimbo la Same Magharibi: Dkt. David Mathayo wa CCM, ameshinda kwa jumla
ya kura 21418, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Christopher Sangweli wa
Chadema, aliyepata kura 15347
Updates: Jimbo la Same Mashariki:Naghenjwa Livingstone Kaboyoka wa Chadema, amembwaga Anne Kilango Malecela kwa jumla ya kura 18836, dhidi ya kura 15539
Updates:Jimbo la Ilemela jijini Mwanza Angelina Mabula wa chama cha Mapinduzi CCM ameshinda kwa kura za
Ubunge, huku Hainess Kiwia kutoka Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA) ameshindwa
kukitetea kiti chake
Updates:Mtwara mjini Maftah Nachuma wa Chama cha CUF ameshinda kwa kura za
Ubunge, huku Asnain Murji kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM) ameshindwa
kukitetea kiti chake
Updates:Jimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro, Freeman Mbowe wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA) atangazwa kuwa Mbunge kwa kupata jumla ya kura
51,124, huku mgombea kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Danstan Mallya
apata jumla ya kura 26,966.
Updates:Jimbo la Mbeya Mjini: Joseph Mbilinyi wa Chadema, ameibuka mshindi kwa
jumla ya kura 97675, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Mwalyengo
Shitambala wa CCM, aliyepata kura 46894
Updates:Jimbo la Kigoma Mjini: Zitto Kabwe wa ACT-Wazalendo, aibuka mshindi kwa
jumla ya kura 31546, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Amani Kaburou wa
CCM, aliyepata kura 16344
Updates:Jimbo la Iramba Magharibi: Mwigulu Nchemba wa CCM, aibuka mshindi kwa
jumla ya kura 54660, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Jesca Kishoa wa
Chadema aliyepata kura 12580
Updates:Jimbo la Ileje: Janet Mbene wa CCM, aibuka mshindi kwa jumla ya kura
27582, dhidi ya mpinzani wake wa karibu Emmanuel Mbuba wa NCCR-Mageuzi,
aliyepata kura 14578
Updates:Jimbo la Mpanda Mjini: Sebastian Kapufi wa CCM, aibuka mshindi kwa jumla
ya kura 29193, dhidi ya mpinzani wake wa karibu wa Chadema Jonas
Kalinde, aliyepata kura 18649
Update:
Anthony Mavunde (CCM) ametangazwa kuwa mshindi wa ubunge Jimbo la
Dodoma Mjini, Joram Hongoli (CCM) akishinda Jimbo la Njombe Kaskazini.
Upadate: Jumanne Kishimba (CCM) ameshinda Jimbo la Kahama Mjini, Steven Masele ameshinda Jimbo la Shinyanga Mjini.Update: Hussein Bashe ameshinda Jimbo la Nzega Mjini na Silvestry Koka ameshinda Jimbo la Kibaha Mjini
Jimbo la Serengeti
Marwa Ryoba (Chadema) amengazwa kuwa mshindi kwa kiti cha Ubunge kupitia
tiketi ya Chadema katika jimbo la Serengeti.Jimbo hilo lilikuwa chini ya Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Stephen Kebwe
Jimbo la Chalinze
Ridhiwani Kikwete wa CCM, aibuka mshindi katika Jimbo la Chalinze Mkoani
Pwani kwa jumla ya kura 52695, dhidi ya Mang’unda Torongei wa Chadema
aliyepata kura 23470
Jimbo la Moshi Mjini
Japhary Michael wa Chadema ameshinda kwa
kura-51647, huku mpinzani wake Davies Mosha wa CCM akipata kura-26920
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Peremiho kwa tiketi ya CCM , Jenister Mhagama ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa jimbo hilo
Jimbo La Arumeru Mashariki
Mgombea Ubunge wa Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chadema , Joshua Nassari ametangazwa rasmi kuwa mshindi wa jimbo hilo
Nassari ameshinda kwa kura 86694, na mpinzani wake wa karibu John Pallangyo wa CCM amepata kura-31847
Nassari ameshinda kwa kura 86694, na mpinzani wake wa karibu John Pallangyo wa CCM amepata kura-31847
Jimbo la Shinyanga
Mgombea
ubunge wa Chadema jimbo Shinyanga Patrobas Katambi amegoma kuendelea
kusikiliza kutangazwa kwa matokeo na msimamizi wa uchaguzi Kalinjuna
Lewis, kwa madai kuwa hana imani na matokeo hayo na kuamua kutoka
ukumbini na wapambe wake wakati matokeo ya kila kituo yakiendelea
kusomwa. Hadi sasa bado hajatangazwa mshindi
Jimbo la Tandahimba
Katika jimbo la Tandahimba mkoani Mtwara, Katani Ahmed Katani wa CUF
ameshinda kiti cha ubunge kwa kura-55156, huku mpinzani wake mkubwa wa
CCM, Shaibu Salimu Likumbo akipata kura-41088
Jimbo la Mbinga Mjini
Mgombea wa Ubunge kupitia CCM jimbo la Mbinga Mjini Sixtus Mapunda ameshinda na kutangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo
Jimbo la Musoma Mjini
Ubunge: Vicent Nyerere(Chadema) 25,549 na Vedastus Mathayo(CCM) 32,836.
Mgombea wa Ubunge kupitia CCM jimbo la Musoma Mjini Vedastus Mathayo ameshinda na kutangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo
Jimbo la Mbinga Vijijini
Mgombea wa Ubunge kupitia CCM jimbo la Mbinga Vijijini Martin Msuha ameshinda na kutangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo
Jimbo la Monduli
Ubunge: Julius Kalanga (Chadema) 35,024 na Namelock Sokoine (CCM) 25,925.
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chadema jimbo la Monduli, Ndugu Julius Kalanga ametangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo
Ubunge: Dk Godwin Mollel (Chadema) 22,746 na Aggrey Mwanry (CCM) 18,584.
Msimamizi
wa Uchaguzi, Rashid Kitambulio amemtangaza Dk Mollel kuwa mshindi wa
jimbo hilo ambalo mbunge wake alikuwa ni Aggrey Mwanry (CCM).
Jimbo la Tunduma
Ubunge: Mwakajoka Frank (Chadema) 32,442, Frank Sichalwe (CCM) 17,220, James Mwakalonge(TLP) 85, Reddy Makuba (ACT Wazalendo) , 319.
Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Tunduma, Halima Mpita ametangaza matokeo hayo.
Jimbo Buyungu
Ubunge: Bilago Samson Chadema), 23,041 na Christopher Chiza(CCM) 22,934
Mgombea ubunge wa Chadema Bilago Samson amefanikiwa kunyakua Jimbo la Buyungu mkoani Kigoma kwa kura 23041.
Jimbo hilo lilikuwa chini ya CCM
kupitia Waziri Christopher Chiza aliyepata kura 22934.
Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Kakonko, Jaina Msangi ametangaza matokeo hayo
Mgombea ubunge wa Chadema Bilago Samson amefanikiwa kunyakua Jimbo la Buyungu mkoani Kigoma kwa kura 23041.
Christopher Chiza |
Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Kakonko, Jaina Msangi ametangaza matokeo hayo
Jimbo la Tarime Mjini
Ubunge: Ester Matiko(Chadema) 20,017, Michael Kembaki(CCM), 14, 025, Deogratias Meck(ACT-Wazalendo) 356.
Jimbo la Lindi Mjini
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM jimbo la Lindi Mjini, Ndugu Hassan Suleiman Kaunje ametangazwa rasmi kuwa mbunge wa jimbo hilo
Maoni
Chapisha Maoni