WHO:WATU MILIONI 1.2 HUFA KILA MWAKA KWA AJALI ZA BARABARANI

WHO:WATU MILIONI 1.2 HUFA KILA MWAKA KWA AJALI ZA BARABARANI

Bara la Afrika ndilo linaongoza kwa vifo vitokanavyo na ajali za barabarani.
Bara la Afrika ndilo linaongoza kwa vifo vitokanavyo na ajali za barabarani.

Shirika la afya duniani-WHO linasema ajali za barabarani zinaendelea kupoteza maisha ya  watu wengi huku idadi ikiwa  milioni 1.25 wanaofariki kila mwaka, ambapo kwa kiasi kikubwa  ajali hizo zinaweza kuzuilika.
Ripoti ambayo kulingana na takwimu zilizokusanywa kutoka nchi 180, inaonesha idadi ya vifo kila mwaka kutokana na ajali za barabarabi inapungua. Ripoti ilitambua hii ni habari njema ambapo matukio haya yanatokea huku idadi ya magari ikiongezeka haraka mno na idadi ya watu inakuwa duniani kote.
Lakini, katika taarifa maalumu, takwimu zilionesha pia kwamba ajali za barabarani ndio namba moja kwa kuongoza  katika vifo miongoni mwa vijana kati ya umri wa miaka 15 na 29. Ripoti ya shirika la afya duniani-WHO pia imegundua mwanya mkubwa katika maeneo ya usalama wa barabarani na vifo kati ya nchi maskini  na tajiri.
Ajali za barabarani huko mashariki ya kati
Ajali za barabarani huko mashariki ya kati
 
Inasema asilimia 90 ya vifo vya ajali za barabarani vinatokea katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati, japokuwa wana asilimia 54 ya magari duniani. Mkuu wa kitengo cha magonjwa yasiyoambukiza katika WHO, Etienne Krug anasema kiwango cha juu kabisa cha vifo vya ajali za  barabarani kipo barani Afrika, ikifuatiwa na mashariki ya kati.
“Afrika ina asilimia mbili pekee ya magari duniani, lakini ina kiwango cha juu sana cha vifo vya barabarani. Baadhi ya nchi kama vile Sweden, Uingereza, Uholanzi na kadhalika wameweza kupunguza viwango vya vifo kwenye barabara zao kwa zaidi ya asilimia 80 katika miongo iliyopita, kwa kutekeleza  hatua  kadhaa zinazoeleweka  vyema. Tunazungumzia kuhusu kuboresha sheria  na kuziimarisha, hususani kwenye vipengele hatari kama vile mwendo kasi, kunywa kilevi na kuendesha, kutumia kofia maalum  helmet unapoendesha pikipiki, kufunga mkanda na kiti cha mtoto”.
Krug alisema katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, nchi 17 zimekuwa na mafanikio  kwa kuweka sharia za usalama barabarani. Anasema majibu ya haraka baada ya ajali pia ni muhimu katika kuokoa maisha.
Ajali za barabarani barani Afrika
Ajali za barabarani barani Afrika
 
Alisema utafiti unaonesha kwamba nusu ya vifo kutokana na majeraha vinaweza kuepukika kama waathirika wanapatiwa huduma bora baada ya ajali.
Ripoti ilionesha kwamba ajali za waendesha baiskeli na watembea kwa miguu zinafikia asilimia 26 ya vifo vyote vitokanavyo na ajali za barabarani, ambapo idadi hii inafikia asilimia 33 huko barani Afrika.
Ripoti pia iligundua kwamba baadhi ya magari yaliyouzwa katika asilimia 80 ya nchi zote yameshindwa kufikia viwango vya msingi vya usalama. Ripoti ilisema hii ni kweli hususani katika nchi maskini sana mahala ambapo takribani asilimia 50 ya milioni 67 ya magari mapya ya abiria ambayo yalitengenezwa mwaka jana.
Share this article :

Maoni