Baraza la madiwani Kiteto kuwa moto

Michael Lepunyati aliyekuwa diwani wa kata kadhaa wilayani Kiteto kwa miaka 20 na sasa amerejea tena kuwa diwani kupitia kata ya Namelock baada ya kumwangusha Yohana Lebakari picha na Mohamed Hamad


HABARI YA MJINI..
Wadadisi wa masuala ya siasa Kiteto wamesema kuwa mwaka huu Baraza la madiwani wilayani Kiteto litakuwa moto baada ya wakongwe kuingia katika baraza hilo

Kubwa ni kila mmoja kutaka kuonyesha uwezo wake na hasa kuwasilisha matatizo ya wananchi wa kata yake waweze kusaidiwa na Halmashauri ya wilaya hususani katika miradi

Miongoni mwa wakongwe hao ni pamoja na Michael Lepunyati CCM huyu amewahi kuwa diwani kwa miaka 20 kuna vijana kama Paulo Tunyoni CCM ambaye ana nguvu kubwa ya kisiasa na mwenye ushawishi mwingi yupo Ngaringe Maitey kata ya Njoro Kidawa kata ya matui  CHADEMA pamoja na wengine wengi

Hitaji la wananchi wa Kiteto sio kuonyesha sura kama wasemavyo wao wanachotaka ni kazi huku wao wakisema "HAPA KAZI TU"

Lakini je watafanikiwa?....mimi na wewe tusubiri baada ya miaka mitano...

Maoni