Ruka hadi kwenye maudhui makuu
Default Yanayojiri Uwanja wa Uhuru: Kuapishwa kwa Dr. Pombe Magufuli kuwa Rais wa Tanzania
Ndugu mtanzania. Leo ni siku ya kihistoria katika nchi yetu
ambapo rais mteule John Joseph Magufuli ataapishwa na kukabidhiwa Nchi
rasmi.
Maandalizi yote muhimu yamekamilika.
Fuatilia uzi huu kwa live updates mwanzo mwisho.
Tukio hili la aina yake litarushwa mubashara na Tbc1,star tv,channel
ten,Azam tv na clouds tv pamoja radio mbalimbali ikiwemo tbc fm.
Stay updated. Stay tuned
*******updates********
- Wageni mbalimbali wanaendelea kuwasili hapa uwanjani.
- Wameingia marais wastaafu akiwemo Benjamin Mkapa,Ally Hassan Mwinyi na
wake zao,mawaziri wakuu wastaafu Msuya na wengineo,Jaji Augustino
Ramadhan na sasa jaji mkuu Othman Chande anaingia na ndio atamuapisha
rais mteule.
- Marais saba wa nchi mbalimbali wanahudhuria tukio hili. Pia waziri mkuu mstaafu wa Kenya Raila Odinga yupo
- Wapo mabalozi wa nchi mbalimbali na wawakilishi wa jumuiya za kimataifa na mashiriki ya UN.
- Spika wa bunge Anne Makinda na naibu spika Job Ndugai wamo.
- Rais wa Zanzibar na delegation yote ya Zanzibar akiwemo Pandu Ameir Kificho wamehudhuria.
- Watu ni wengi kweli kweli
RAIS MTEULE KATIKA KILA TUKIO MUHIMU MVUA ILINYESHA IKIWEMO LEO. ISHARA YA BARAKA NA UTAWALA HALALI WA RIDHAA YA WANANCHI.
- Vikosi vya majeshi ya wananchi ya tanzania viko tayari kwa gwaride maalum.
- Wabunge wateule wa Jamhuri ya Muungano wameshaketi tayari.
- Jaji Mkuu Othman Chande ndio anawasili sasa hivi.
- Bendera ya Rais wa sasa itashushwa na kuashiria ukomo wa serikali ya
awamu ya nne na Rais wa awamu ya tano atakapoapishwa bendera ya taifa
itapandishwa.
- Anaingia mke wa Rais Mteule Mama Janet Magufuli
- Wapo viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa
- Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amewasili hivi punde.
- Rais Jakob Zuma wa Afrika Kusini pia naye amefika.
-Maandamano rasmi ya kuelekea Jukwaa Maalum la Kuapishwa Rais mteule
yataongozwa na Jaji Mkuu,Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na Katibu
Mkuu Kiongozi.
- Tukio linalofuata ataingia Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote ya Tanzania, Mh. Jakaya Mrisho Kikwete.
- Rais mteule Dr. Magufuli ameelekea jukwaa maalum la kiapo.
- Rais anakagua gwaride kwa mara ya mwisho kisha ataenda jukwaa la
kuapisha na mizinga 21 inapigwa, kisha bendera ya serikali ya awamu ya
nne itashushwa.
-Wimbo wa taifa unaimbwa.
Bendera ya serikali ya awamu ya nne inashushwa kuashiria mwisho wa utawala wa awamu ya nne.
TUKIO LA KUAPISHWA MAGUFULI LINAENDELEA.
- Rais anayemaliza muda wake akiwa na makamu wake wanasaini kukubali
kwao kukaa benchi na kukabidhi nchi rasmi kwa Rais wa Awamu ya Tano.
***UPDATES***
- Rais wa awamu ya Tano na makamu wake wameshakula kiapo, sasa ni sala kutoka kwa viongozi mbalimbali wa dini.
****updates*****
RAIS WA AWAMU YA TANO WA TANZANIA JOHN MAGUFULI ANAPIGIWA MIZINGA 21 YA UTIIFU YA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA.
UPdates******
RAIS JOHN P MAGUFULI ANAKAGUA GWARIDE LA TZ LIKIWA KATIKA UMBO LA ALFA
KUASHIRIA MWANZO WA SERIKALI MPYA. Rais amemaliza kukagua gwaride na
sasa amepanda jukwaa kuu
Hii mvua inaashiria nini kwa Dr. Magufuli?
Siku ya kupiga kura ilinyesha Chato.
Maoni
Chapisha Maoni