John
Pombe Joseph Magufuli (56) ameapishwa mapema leo kuwa Rais wa tano wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es
Salaam.
Baada
ya kuapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Jaji Othaman Chande Rais John
Magufuli alitoa neno la shukrani kwa watanzania na kuwataka washindani
wake saba waliokuwa wakichuana katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba
25 mwaka huu kuweka itikadi za vyama pembeni na kushirikiana kwa
kufanya kazi kwa maslahi ya Taifa zima.
Amesema
kuwa kwa kuwa uchaguzi umekwisha ni vema viongozi hao wakaweka
itikadi,maslahi na matakwa yao binasfi kando na kuungana nae kujenga
taifa imara.
“Uchaguzi
umekwisha na Rais ni mimi John Magufuli sasa ni wakati wa kufanya kazi
tu…na nitafanya kazi kwa nguvu zangu zote na kwa kumtanguliza Mungu
mbele,”alisema Rais
Magufuli.
Ameongeza
kuwa dhamana waliyopata kutoka kwa watanzania ni kubwa sana na ni
jukumu la Serikali ya awamu ya tano kuhakikisha wanatekeleza ahadi zote
walizotoa wakati wa kampeni walipokuwa wakiomba ridhaa ya kuliongoza taifa.
Rais
Magufuli hakusita kumshukuru Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin
Wiliam Mkapa ambaye alimteua kuwa waziri wa Ujenzi kwa kipindi chake
chote cha miaka 10 wakati huo akiwa na umri wa miaka 35 tu.
Pia
alimshukuru Rais Mstafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete
ambaye naye alimchagua kuwa waziri katika Serikali yake na baadae akiwa
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumpa dhamana ya kupeperusha
bendera ya chama hico na kuwa Rais wa tano wa Jamhuri ya Muungano ya
watu wa Tanzania.
"Magufuli ni nani mpaka achaguliwe na kuaminiwa kuliongoza Taifa hili?," alihoji na kuendelea kusema.. "Nakosa maneno mazuri ya kuongea lakini leo sio sehemu ya kutoa hutuba nipo hapa kushukuru tu"
Mpekuzi blog
Maoni
Chapisha Maoni