KAMATI KUU YA CCM KUKUTANA KESHO JUMAPILI DODOMA



 
 
 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM inatarajiwa kufanya kikao chake cha siku moja mjini Dodoma kesho Novemba 15, 2015 kujadili majina ya wana-CCM walioomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea Uspika na Unaibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kamati Kuu itafanya kikao chake kesho saa sita kamili mchana chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Kikao cha Kamati Kuu kitafuatiwa na Kikao cha Kamati ya Wabunge wote wa CCM kitakachofanyika Novemba 16, 2015 saa nne asubuhi katika ofisi za Makao Makuu ya CCM Dodoma.
Imetolewa na:-
Nape Moses Nnauye
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
14/11/2015

Maoni