Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Kikwete aingia mtaani


Raisi mstaafu,Jakaya Mrisho Kikwete,jana aliingia mtaani na kufanya shopping Mliman City.

======================
KWA mara ya kwanza tangu aondoke madarakani mwanzoni mwa mwezi huu, jana Rais Jakaya Kikwete alionekana akifanya manunuzi katika maduka yaliyopo jengo la Mlimani City, jijini Dar es Salaam.

Kikwete, ambaye alikuwa amevalia suti maarufu kama ?kaunda suti? yenye rangi nyeusi, alionekana akiingia katika viunga vya Mlimani City saa 5:00.

MTANZANIA Jumamosi ambalo lilikuwepo katika viunga hivyo vya Mlimani City lilishuhudia Kikwete akiwasili katika maeneo hayo akiwa katika msafara wa magari manne na pikipiki moja.

Rais huyo mstaafu pia alikuwa ameambatana na mkewe, Salma Kikwete, aliyekuwa amevalia mavazi ya kitenge pamoja na walinzi wao wanne.

Hatua hiyo ilionekana kushangaza baadhi ya watu waliokuwepo katika maeneo hayo, huku wengi wao wakionekana kutaka kumsalimia.

MTANZANIA Jumamosi ambalo muda wote lilikuwa likimfuatilia Rais Kikwete na mke wake, lilishuhudia wakiingia katika maduka ya Game na kufanya manunuzi kwa dakika zisizopungua 10 hadi 15 na baadaye kutoka nje na walinzi wake wakionekana kubeba mifuko iliyokuwa na bidhaa walizonunua.

Kama ilivyo hulka ya Rais Kikwete alipotoka nje ya duka hilo alianza kusalimiana na mtu mmoja ambaye alionekana kufahamiana naye.

Hatua hiyo ilimpa fursa ya kuwasalimia watu wengine waliokuwa karibu na tawi la benki moja.

Baada ya hapo msafara wake uliondoka na kuelekea Barabara ya Sam Nujoma.

Tangu achaguliwe kuwa rais mwaka 2005 itifaki na majukumu yake ya urais yalikuwa yakimbana Rais Kikwete na hivyo kushindwa mambo yake binafsi kama walivyo raia wengine.

Pamoja na kwamba Kikwete sasa ni raia, lakini kutokana na wadhifa aliowahi kuushika wa urais bado halingani na raia wengine wa kawaida, ingawaje majukumu ya urais yamepungua na hivyo kumpa fursa ya kutembea katika maeneo ya wazi na kufanya matumizi ya kawaida kama alivyofanya jana.

Tangu alipoachia kiti cha urais na kumkabidhi Dk. John Magufuli baada ya kuapishwa Novemba 5, Kikwete amekuwa akiishi nyumbani kwake Msoga, mkoani Pwani.

Rais Kikwete aliondoka rasmi Ikulu na familia yake Ijumaa iliyopita Novemba 6 na kuanza maisha mapya kijijini kwake huko.

Chanzo: Mtanzania

Maoni