TAHADHARI KIPINDUPINDI KITETO NA HII NI PICHA ILIYOPIGWA DAR JUU YA TAHADHARI HIYO
Hofu ya ugonjwa wa Kipindupindu wilayani Kiteto imezagaa kila kona, baada ya wagonjwa wanne kulazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto, huku viongozi wa wilaya wakikanusha kuwepo kwa ugonjwa huo, hata hivyo taarifa za uhakika zinasema kuwa sampuli iliyopelekwa Dodoma imethibitisha kuwepo kwa miongoni mwa wagonjwa hao kuwa na ugonjwa wa kipindupindu
Uongozi wa Hospitali ya Wilaya ya Kiteto umeitwa mkoani Manyara kwaajili ya zoezi zima la kukabiliana na kipindupindu huku ikidaiwa kutokuwepo kwa tahadhari ya kutosha pamoja na madawa kwaajili ya tatizo hilo,Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa za uhakikia kutoka kwa wahusika wa Hospitali ya Wilaya ya Kiteto zinasema kambi iliyothibitishwa kuweka wagonjwa hao ni Zahanati ya Bwagamoyo iliyopo kata ya Bwagamoyo
Hakuna mtu aliyeripotiwa kupoteza maisha hadi sasa...

Maoni
Chapisha Maoni