MAGUFULI TAYARI ANA SPIKA,NAIU SPIKA NA WAZIRI MKUU,SOMA WASIFU ZAO HAPA


tulia
Dkt. Tulia Ackson Mwansasu (Naibu Spika wa Bunge 2015-2020).
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limempitisha Dkt. Tulia Ackson Mwansasu kuwa Naibu Spika wa Bunge, kwa kura 250 sawa na 71.2% dhidi ya mpinzani wake, Mh. Magdalena Sakaya aliepata kura 101 sawa na 28.8%. 
kasim
Kassim Majaliwa (Waziri Mkuu mpya wa Tanzania 2015-2020)
 
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, muda mfupi uliopita limepitisha jina la Mbunge wa Jimbo la Rwangwa, Mh. Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Serikali ya awamu ya tano baada ya jina lake kupelekwa Bungeni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
 
Mh. Majaliwa amepitishwa kwa kura 258 sawa na asilimia 73.5% ya kura zote za ndio.

Maoni